Upinzani unaokuzwa na mashabiki kati ya Diamond Platnumz na Ali Kiba kwenye mitandao ya kijamii umepelekea Mastaa wa Tanzania kuanza kujitokeza hadharani na kuwaweka mashabiki hawa sawa kwa kuamini wamevuka mipaka kwenye ushabiki.
Mtangazaji wa TV show ya Mkasi Salama Jabir na msanii mkongwe bongoflevani Solo Thang ni miongoni mwa waliozipaza sauti zao June 30 2015.
Kupitia kwenye ukurasa wa twitter Salama Jabir aliandika ‘Wabongo
tumekua wakosoaji mpaka wasanii wanajishtukia, hakuna “zuri kabisa”
kwenye macho yetu… tuwaache wasanii wawe “Wasanii” nadhani!
‘Jana tulikua tunaongea na wana job, Ali Kiba hakuwa mtu wa vioo vikali, yeye alikuwa anatoa audio kali na video ya Mwananchi kamaliza, zama zimebadilika mpaka anakwea pipa kwenda kutoa kideo kikaaali tushukuru, kapendeza, rangi nzuri! mengine tuyaache..’ kauli ya Salama Jabiri
Upinzani
huo ulioanzishwa na makundi yanayojiita (TeamAliKiba na TeamDiamond)
yalimkwaza pia mkongwe wa Hip Hop Solo Thang na kuandika..’Ukiweka
habari au picha au muziki wa msanii muyu mashabiki wa yule
wanakutukana! kwanini? ? hii burudani tu isiwe uhasama, tujivunie sanaa
yetu..’
Yeah I like #ALI KIBA and #DIMOND music, why do I have to choose a side??,, Both are TANZANIAN ARTIST,, BOTH ARE TALENTED #SupporturOWN #TZ
— SOLO THANG~S.U.M.U (@solothang) June 30, 2015
Ukiweka habari au picha au Music wa msanii Huyu #mashabiki wa yule wanakutukana! Why? ?hii #Burudani tu isiwe Uhasama, tujivunie sanaa yetu!
— SOLO THANG~S.U.M.U (@solothang) June 30, 2015
Wabongo Tumekua Wakosoaji Mpaka Wasanii Wanajishtukia, Hakuna "Zuri Kabisa" Kwenye Macho Yetu... Tuwaache Wasanii Wawe "Wasanii" Nadhani!
— Salama Zalhata Jabir (@EceJay) June 30, 2015
...Zama Zimebadilika Mpaka Anakwea Pipa Kwenda Kutoa Kideo Kikaaali Tushukuru, Kapendeza, Rangi Nzuri! Mengine Tuyaache!
— Salama Zalhata Jabir (@EceJay) June 30, 2015
...Zama Zimebadilika Mpaka Anakwea Pipa Kwenda Kutoa Kideo Kikaaali Tushukuru, Kapendeza, Rangi Nzuri! Mengine Tuyaache!
— Salama Zalhata Jabir (@EceJay) June 30, 2015
0 comments:
Post a Comment