Wakati unapoangazia swala la utengezaji magari mataifa ya Afrika kwa kawaida hayaorodheshwi katika swala hilo.
Lakini
hilo sasa huenda likabadilika kufuatia kuwasili kwa kampuni ya magari
ya Ghana Kantanka ambayo hivi karibuni yataanza kuingia katika soko.Miongoni mwa magari ya kampuni hiyo ni lile la lita mbili aina ya 4 by 4 ambalo linatarajiwa kuuzwa kwa takriban pauni 14,000.
Lakini je,kampuni hiyo itaweza kukabiliana na ushindani mkubwa kutoka kwa magari kama vile Toyota,Land Rover na BMW?.
Kwadwo sarfo ni mwana wa mmiliki wa magari hayo.
Babaake ni m'bunifu ambaye pia ni kiongozi wa dini.Hupata fedha kutokana na kilimo na uchimbaji.
Magari ya Kantanka yanafananishwa na magari makubwa kama vile Toyota Prado ama MItsubishi Pajero.
Mbele ya gari hilo kuna michoro ya kucha za chui pamoja na nembo ya kampuni hiyo ya nyota ya Afrika.
Kulingana na raia mmoja wa Ghana uvumbuzi kama huo haujafanyika nchini humo.
Tunapenda kununua bidhaa kutoka nje kwa hivyo italazimu kufanyika kwa mauzo ya ziada kwa gari hizi za kantanka kukubalika.
Profesa Robert Ebo Hinson ambaye ni mkuu wa kitengo cha mauzo katika chuo kikuu cha Ghana:Nadhani kile kilichotokea hapo awali ni kwamba tumefanywa tuamini kwamba kile kinachotengezwa katika mataifa ya magharibi ni
bora zaidi kwa sababu zote zile.
Wakati mwengine bidhaa zinazotengezwa kutoka Ghana haziwezi kudumu.
Serikali ya Ghana inaelewa kikwazo hicho na tayari imeanzisha kampeni kubwa ya kuwafanya wakaazi kununua bidhaa zinazotengezwa nchini humo.
Waziri wa biashara daktari Ekow Spio Gabrah anaongoza kampeni hiyo na anasema:Nitaendesha moja ya magari haya,kwa kweli niliketia gari moja wakati lilipokuwa likitengezwa na nafurahi kuwa na moja kama gari langu rasmi.
Magari
Waziri na rais wana uwezo wa kuendesha magari hayo kwa gharama ya walipa ushuru.
Lakini je,raia wataweza kutumia fedha zao wenyewe kulipia gharama za kulinunua gari hilo?
Inaonekana kwamba raia wengi kama alivyodai hapo awali Professa wana wasiwasi kuhusu usalama wa gari hilo na kudumu kwake.
Je, unadhani wasiwasi huo huenda ukaathiri uzalishaji wa magari hayo? Kulingana na Kwadwo Sarfo gari hilo la kwanza kutengezwa nchini Ghana litapata umaarufu.
CHANZO -BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment