Hit maker wa ‘Hakunaga’, Suma Lee amesema kuwa hatafanya tena muziki kwasababu ameachana kabisa na maisha hayo.
Suma ambaye alitengeneza pesa nyingi kupitia hit yake ya ‘Hakunaga’,
amesema kuwa hana mpango wa kuzitoa nyimbo zake zilizoko studio ambazo
hazijatoka.
“sifanyi tena muziki na nimeachana kabisa na maisha hayo, na nyimbo
zote zilizobaki studio nimezisimamisha zisitoke baada ya kuzilipia, “
Alisema Suma.
“kuna wimbo mmoja nimefanya na Cp ambao ndio ulikuwa wa kurudisha
kundi la Parklane, pia nimeuzuia, labda Cp auchukue yeye.Kilichobaki ni
kuwaombea wazazi wetu waliotutangulia, wengine walikuwa hawataki tufanye
kazi hizi, kwa kuwa hawapo na hakuna wakutukataza tena, bora tukae na
kuwaombea.”
Home / Bongo yetu /
isikupite /
Ma Star wetu
/ Suma Lee: Nyimbo zote zilizobaki studio nimezisimamisha zisitoke, sifanyi tena muziki
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment