Umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi, Nato wametoa
picha za satelaiti zinazowaonyesha askari wa Urusi wakiwa na silaha
ndani ya nchi ya Ukraine kuwasaidia waasi wanaotaka kujitenga kupambana
na majeshi ya serikali ya Ukraine.
PICHA: Raisi wa Ukrain Viktor F. Yanukovych
PICHA:RAISI WA URUSI Vladimir Putin
PICHA: Raisi wa Ukrain Viktor F. Yanukovych
PICHA:RAISI WA URUSI Vladimir Putin
Mapema, waasi waliteka mji wa pwani ya Novoazovsk ulioko kusini.
Watu wapatao 2,119 wameuawa katika mapigano yaliyodumu kwa miezi minne.
Katika taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Marekani, Bwana Obama amesema waasi katika eneo hilo wamepatiwa mafunzo, silaha na kufadhiliwa na Urusi.
Hata hivyo, kauli ya Bwana Obama imekuwa na mashaka aliposema Marekani na NATO hawatachukua hatua za kijeshi dhidi ya waasi nchini Ukraine.
Huku kukiwa na shutuma kutoka mataifa ya magharibi, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limefanya mkutano wa dharura mjini New York kujadili mgogoro wa Ukraine.
"Urusi inatakiwa kuacha kudanganya na iache kuchochea mgogoro huu," balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Samantha Power,ameliambia Baraza la Usalama.
Naye balozi wa Uingereza Sir Mark Lyall Grant amesema Urusi ilikuwa na hatia "kwa ukiukaji wa wazi wa nchi huru ya Ukraine", akisema kuwa mgogoro huo "usingekuwepo" kama Urusi isingeingia moja kwa moja kuwasaidia waasi.
0 comments:
Post a Comment