Msanii wa Kundi la Orijino Komedi, Mujuni Sylivery aka Mpoki moja ya vitu ambavyo aliwahi kuvifanya katika kazi yake ya uchekeshaji ni pamoja na kuigiza sauti ya marehemu, Kapteni John KOMBA ambaye amefariki February 28.
Leo Mpoki amesikika kwenye Leo Tena @CloudsFM, alianza kuzungumzia namna alivyopokea taarifa za msiba huo; “..Mtu akishatoweka kwenye ulimwengu akifariki dunia inauma kwa sababu mtu unayempoteza leo huwezi kumpata tena.. lakini ukimpoteza mbuzi utaenda Vingunguti utamnunua na sherehe itaendelea.. Kitendo cha kufariki mtu yoyote hata kama hajulikani ni pengo kubwa tu”
“Imeniathiri kwa kisanii kwa kuwa nilikuwa namuwezea, kidogo alikuwa hapendi lakini ilivyokuja akatulia.. Watu wakamwambia bwana hawa watoto tu.. Ukimuiga mtu ana mazuri huwezi kumuiga kwa mabaya tu.. ana mazuri yake..Ikanipa wigo mpana kwenye kazi yangu ya kubuni sauti yake, vitendo..“
“mwisho wa siku kaondoka pengo lake halitozibika.. Kama kuna la kufanya kuhusu yeye kwa kumuenzi sitokuwa nyuma, nitafanya ili mradi lisimvunjie heshima Marehemu, familia yake, jamii, viongozi wenzake Bungeni na watu wote ambao kawaacha kwenye jimbo lake sasa hivi wapweke..“
Isikilize sauti yote hapa pamoja na sauti ya Mpoki akimuiga marehemu Kapteni Komba.
Hii ilikuwa Interview aliyofanyiwa Kapteni Komba mwaka 2013, ishu ya Mpoki kumuiga aliizungumzia hapa pia..
0 comments:
Post a Comment