Sauti ya KAJALA, SHAMSA FORD, QUEEN DARLEEN na mtoto wa Marehemu John KOMBA kwenye 255..

IMG_2970
Sauti ya Shamsa Ford na Kajala waigizaji wa Bongo Movie, Queen Darleen msanii wa Bongo Fleva wamesikika kwenye story ya kwanza kwenye 255 kuhusu project yao ya wimbo wa kupambana na mauaji ya albino TZ.
Shamsa amesema manager wake alimfikishia taarifa za idea hiyo naye akakubaliana nayo.
Kajala amesema alipewa taarifa na manager wake, wakakubaliana kuungana na wasanii wengine wa kike ili kuufanya wimbo huo.
Queen Darleen amesema anaamini kuungana huko ni kitu endelevu kwa kuwa wanawake ni walezi wa familia ambao mambo mengi yanakuwa yanawahusu moja kwa moja.
Mtoto wa Marehemu Kapteni John Komba, Herman John Komba ambaye amesema siku nzima ya Jumamosi February 28 alikuwa pamoja na baba yake wakazunguka maeneo mbalimbali na baadaye wakarudi nyumbani akiwa mzima kabisa, hali ilibadilika muda mfupi baadaye ambapo walipofika njiani wakati wakimpeleka Hospitali alikata kauli.
Mazishi ya Mbunge huyo yatafanyika Mkoa wa Ruvuma ambako mtoto huyo wa Marehemu amesema baba yake aliagiza kama akifariki azikwe huko.
Bonyeza play hapa uisikilize 255 yote..

Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment