Mwenyekiti
wa Bunge Maalum la Katiba, Mh. Samuel Sitta (kulia), akisisitiza jambo
kwa wawakilishi wa mashirikisho ya sanaa mjini Dodoma hivi karibuni.
Mashirikisho hayo yamekuwa yakipambana kufa na kupona kuhakikisha katiba
mpya inatambue wasanii kama kundi maalum na pia ilinde mali
zisizoshikika yaani miliki bunifu (intellectual property). Maoni ya
mashirikisho hayo yalishatolewa katika hatua za awali za utoaji maoni na
pia kupitia mabaraza lakini kwa bahati mbaya, hayakujumuishwa katika
rasimu. Waliokaa
kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki Tanzania, Bw.
John Kitime, Rais wa Shirikisho la Filamu, Bw. Simon Mwakifwamba na
Makamu mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Bi. Samia Suluhu Hassan. (Picha zote kwa hisani ya ofisi ya Bunge la Katiba).
Mwenyekiti
wa Bunge Maalum la Katiba, Mh. Samuel Sitta akikabidhiwa nyaraka yenye
hoja ya uzengezi (lobbying) kutoka kwa kiongozi wa msafara wa
mashirikisho ya sanaa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la
Filamu nchini, Bw. Simon Mwakifamba, mjini Dodoma hivi karibuni. Makamu Mwenyekiti wa Kamati namba tano ya Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Assumpter Mshama, akishibishwa hoja za
kina kwa nini wasanii wanataka katiba mpya itambue wasanii kuwa kundi
maalum na pia ilinde mali isiyoshikika au kwa lugha nyepesi miliki
bunifu (intellectual property) toka kwa Mwenyekiti wa Mtandao wa
Wanamuziki Tanzania, Bw. John Kitime, mjini Dodoma hivi karibuni.
0 comments:
Post a Comment