Mayweather apokonywa mkanda wa WBO alioshinda kwenye pambano lake na Pacquiao

Floyd Mayweather amepokonywa mkanda wa WBO alioshinda kwenye pambano lake na Manny Pacquiao mwezi May.
mayweather-pacquiao-050315-getty-ftrjpg_t6stlfhcwee616mai4sjautnc
Bondia huyo alishindwa kulipa gharama za kutambuliwa kwa pambano hilo (sanctioning fee) ambayo ni dola $200,000 ambapo mwisho wa kulipa ilikuwa ni July 3.
Bondia Timothy Bradley ndiye ataushikilia mkanda huo kwa sasa.
“The WBO World Championship Committee is allowed no other alternative but to cease to recognize Mr Floyd Mayweather Jr as the WBO welterweight champion of the world and vacate his title,” yanasema maelezo kwenye mtandao wa wboboxing.com.
Mayweather anayeshikilia mikanda mingine ya WBA na WBC ana hadi July 20 kuweza kuukatia rufaa uamuzi huo.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment