WASTARA AMLILIA SAJUKI

Image result for wastara sajuki



Nukuu kotaka instagram page ya waastara


@wastara84





Naanza kwa kumshukuru mungu wangu anaenipa pumzi ya bule mpaka mda huu Sina budi kusema haya nitakayoyasema kwa ajili mwaka mpya unaonza kesho Ni miaka 5 na miezi 6 leo imetimia toka furaha yangu ilipoingia dosari Mungu alinipa mtu wa kunipa furaha kwasababu kilakitu Alhamdulilah nilikuwanacho kulingana na nafasi yangu lakini sikuwa na furaha lakini furaha hiyo aikudumu nakumbuka ilikuwa mwezi 6/ 2011 marehemu sajuki alipoanza kuumwa ndipo furaha ilipoanza kupotea kwa sababu sikupata nafuu wala moyo wangu kupumzika mpaka leo tarehe 31/12/2016 nimejaribu kutafuta furaha kila sehemu kila njia ila imeshindikana, kuishi katika mazingira hayo kwa mtu mwengine angekuwa kama kizee hata kuchana nywele ingekuwa shida ila katika maisha ya maumivu na sajuki siku moja aliniambia mke wangu mi naumwa ila sipendi kukuona ukiwa mchafu na pia usinizuie kwenda kokote sababu nitakufa siku yoyote tutumie mda uliobakia kufanya kile kitu moyo unataka Nami kwasasa naishi hivyo nahisi mauti yapo karibu yangu sana hivyo kile moyo wangu unataka ndicho nakifanya hata moyo ukiniambia inuka na maumivu yako nipeleke baharin basi naupeleka uko ukisema nipeleke disco naupeleka uko ukisema nikakeshe msikitin naupeleka uko hivyo sitabariki na sipendi kuishi ili mtu anione nina maumivu nalazimisha furaha japo aipo hivyo mnisamehe wale wote msionielewa kokote mkinikuta mniche tu sifanyi kitu kumkera mtu i need peace of mind,moyo wangu maskin unanivuja damu kilasiku natamani nifanye lolote ili upumue hakuna kitu kibaya kama kupoteza furaha na tumain unaishi kama uko dunia ya peke yako nimeongea haya ili muelewe hisia zangu kuwa hata ukiongea kitu ambacho sijakifanya sihusiki au kunitafsiri vibaya naumia mara 2 nahisi kama na wew ni mmoja ya wale wasiopoenda kuona nikifurahia uwepo wangu duniani Viongozi wangu ndugu jamaa wasanii wenzengu na mshabiki wangu nawaomba kwa pamoja mpige goti kuniombea 2017 moyo wangu upate furaha ya kudumu upate dawa ya maumivu upate tabasamu la kweli na sio feki ninalotoa sasa aniondoshee maradhi yote moyo wangu unahitaji furaha masikin mwaka 2017 uwe na neema kwetu sote ameen
A photo posted by Wastara Sajuki (@wastara84) on
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment