Taarifa zimedai kuwa miongoni mwa watu waliouawa ni pamoja na askari wanne, mgambo mmoja, raia wawili na jambazi mmoja.
Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa chingaone blog, Jennifer Livigha hiki ndicho kilichotokea:
Nimepita eneo la tukio na kujaribu kupata habari ila bado pagumu ila nimepata taarifa zifuatazo: Waliouwawa ni watu saba wakiwemo polisi 4. Kati ya watu 7 waliuwawa kuna mwanamke mmoja aliyeletwa kituoni hapo na mgambo muda mfupi kabla ya tukio. Kati ya waliowawa mmoja ni dereva wa bodaboda na muuza genge wanaofanya biashara zao maeneo jirani na kituo. Inasemekana baada ya majambazi hayo kumaliza uvamizi huo walimuua dereva wa bodaboda na muuza genge waliokuwa maeneo jirani. Silaha aina ya SMG 15 zinakisiwa kuibiwa. Majambazi hayo yalitumia gari aina ya defender.
Mkuu wa Jeshi la Poilisi nchini, Ernest Mangu akiongea na wanahabari mapema leo.
Askari wanne na raia watatu wamefariki Dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kituo kidogo cha Polisi cha Stakishari, Ukonga jijini Dar kuvamiwa na watu wanaosadikika majambazi.
Majambazi hao waliokadiriwa kua wanane walivamia kituo hicho mida ya saa 4 usku Jumapili July 12, 2015 usiku wa kuamkia leo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Enerst Mangu amesema lengo la majambazi hayo ilikua ni kuiba silaha zilizokuwepo kwenye kituo hicho kidogo cha Polisi cha Stakishari, Ukonga jijini Dar es salaam.
Akiongean na wanahabari IGP Ernest Mangu amewaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi katika kusaidia kuwakamata majambazi hao na hatimae kufikishwa katika mkono wa sheria.
IGP Enerst Mangu aliwaambia wanahabari, Jeshi la Polisi litaongeza ulinzi katika vituo hivyo kwa lengo la kuimarisha usalama wa wananchi wake.

“Poleni wote mliofikwa na maafa haya. Mungu azipe Faraja familia ambazo zimepoteza ndugu zao. This happened just next to the house that I grew up in…. My family is okay, but the whole STAKISHARI UKONGA is shocked and shaken. How can we feel safe, if people whom we depend on for our safety are also endangered?! #StakishariUkonga #PolicePostAttack #RIP #WatuWawajibishwe #Unacceptable
0 comments:
Post a Comment