NI taharuki iliyojaa majonzi na simanzi kufuatia Jeshi la Wananchi wa Tanzania ‘JWTZ’ Kikosi cha CMTU jijini Dar kuondokewa na mpiganaji wake, Sajenti Yohana Lugendo Gweso (40) ambaye alikuwa milionea aliyepigwa risasi sita mwilini na kufariki dunia papo hapo.
Mwili wa marehemu Sajenti Yohana Lugendo Gweso (40) wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ‘JWTZ’ Kikosi cha CMTU ukiwa kwenye jeneza.
Tukio hilo la kusikitisha, lilijiri saa 1:45 usiku wa Septemba 22,
mwaka huu, Ukonga Babana ndani ya baa maarufu ijulikanayo kwa jina la
Super Karatu.
UWAZI HATUA KWA HATUA
Kufuatia tukio hilo, Uwazi kama kawaida yake lilifuatilia kwa kina ili kubaini yaliyofichika nyuma ya pazia kama siyo sirini!
Kufuatia tukio hilo, Uwazi kama kawaida yake lilifuatilia kwa kina ili kubaini yaliyofichika nyuma ya pazia kama siyo sirini!
Gari kubwa la jeshi lililoandaliwa kwa ajili ya kuuchukua mwili wa marehemu Sajenti Yohana Lugendo Gweso kwenda Bunda kwa mazishi.
Habari
zilizopatikana zilidai kuwa, siku ya tukio, marehemu Gweso alipigiwa
simu akiwa njiani kurudi nyumbani kwake akitokea Hospitali ya Dar Group
iliyoko Tazara jijini Dar.
Ikadaiwa kuwa, baada ya kupata simu hiyo alifika kwanza nyumbani kwake Gongo la Mboto kambini.
“Alipofika alikula chakula cha mchana kisha alipumzika. Ilipofika saa 11 jioni aliondoka kwenda kwenye shughuli zake za biashara. “Alipokuwa huko inadaiwa alipigiwa simu na mtu huyo wa mwanzo na kupanga sehemu ya kukutania ambapo ilikuwa ni hapo baa,” alisema ndugu mmoja akiomba kusitiriwa jina lake.
AONDOKA NA NDUGU“Alipofika alikula chakula cha mchana kisha alipumzika. Ilipofika saa 11 jioni aliondoka kwenda kwenye shughuli zake za biashara. “Alipokuwa huko inadaiwa alipigiwa simu na mtu huyo wa mwanzo na kupanga sehemu ya kukutania ambapo ilikuwa ni hapo baa,” alisema ndugu mmoja akiomba kusitiriwa jina lake.
Mpiganaji huyo inadaiwa wakati anatoka katika biashara zake alikuwa na mtoto wa dada yake aliyetajwa kwa jina moja la Frank ambaye alikuwa akisimamia hesebu zote za biashara. Siku hiyo walikuwa wamekusanya kiasi cha shilingi milioni 42.
Ikadaiwa kuwa, walipofika Banana kabla ya kuingia Baa ya Super Karatu, marehemu ambaye alikuwa akiendesha gari lake aina ya Toyota
Prado lenye namba za usajili T 855 BWK, alimshusha Frank na kumtaka
atangulie nyumbani kwani alihitaji kwenda Super Karatu kukutana na
mwanamke huyo ambaye baadhi ya watu wanadai ni mweupe, mnene aliyepanda
hewani (mrefu).
Mjane
(mwenye kilemba cheupe) wa marehemu Sajenti Yohana Lugendo Gweso
akisaidiwa na ndugu wa karibu kuingia kwenye gari lililoandaliwa kwa
ajili ya safari.
AFIKA ENEO LA MAUAJI YAKEHabari zaidi zinasema kuwa, marehemu aliwasili kwenye baa hiyo saa 1 usiku na kutafuta maegesho. Alishuka na kuanza kutembea, lakini ghafla kwa nyuma aliitwa na watu wawili ambao walimuita; “Gweso tuko hapa.”
Wakati anageuka kuwafuata watu hao, watu wengine walianza kuvunja gari lake vioo hivyo alirudi mbio ili kujua nini kinaendelea.
“Kumbe wau hao walikuwa kundi moja na mashambulizi ya risasi yalianzia hapo.
“Marehemu alimiminiwa risasi sita mwilini, alipigwa kichwani, nyingine kifuani na walimchukulia fedha zote milioni 42 na bastola yake kisha wakatokomea,” aliendelea kusema ndugu huyo.
MWILI WAKUTWA CHINI“Kumbe wau hao walikuwa kundi moja na mashambulizi ya risasi yalianzia hapo.
“Marehemu alimiminiwa risasi sita mwilini, alipigwa kichwani, nyingine kifuani na walimchukulia fedha zote milioni 42 na bastola yake kisha wakatokomea,” aliendelea kusema ndugu huyo.
Baada ya tuko hilo ndugu, jamaa na marafiki walijulishwa kuhusiana na kifo cha mjeshi huyo ambapo walifika na kuuchukua mwili wa marehemu hadi Hospitali ya Rufaa ya Lugalo jijini Dar kwa ajili ya kuuhifadhi.
UTAJIRI WA MAREHEMU
Mpaka kifo chake, marehemu Gweso alikuwa akimiliki magari manne ya kisasa, Toyota Prado (alikuwa nalo siku ya tukio), Toyota Verossa, Suzuki Vitara na VRS.
Aidha, alikuwa akimiliki biashara mbalimbali kama vile baa, duka la bia za jumla na nyumba ya kulala wageni. Vyote vipo Ukonga, Dar.
Baadhi ya waombolezaji siku ya msiba walimtaja marehemu kuwa mwanajeshi milionea aliyehakikisha anapiga hatua kwa biashara kila kukicha.Mpaka kifo chake, marehemu Gweso alikuwa akimiliki magari manne ya kisasa, Toyota Prado (alikuwa nalo siku ya tukio), Toyota Verossa, Suzuki Vitara na VRS.
Aidha, alikuwa akimiliki biashara mbalimbali kama vile baa, duka la bia za jumla na nyumba ya kulala wageni. Vyote vipo Ukonga, Dar.
ALIANZA KUWINDWA MWAKA 2008
Habari zaidi zinadai kuwa, marehemu alianza kuwindwa mwaka 2008 ambapo watu wasiojulikana majina, sura wala nia yao, walivamia nyumbani kwake, Banana (uswahilini) na kumpiga risasi mtoto wa dada yake na kufariki dunia papo hapo.
Inadaiwa watu hao waliamini mtoto huyo ni Gweso mwenyewe lakni yeye
hakuwepo. Kufuatia tukio hilo, marehemu aliomba kuhamia kambini kwa
usalama wake hadi kifo kilipomkuta hivi karibuni.Habari zaidi zinadai kuwa, marehemu alianza kuwindwa mwaka 2008 ambapo watu wasiojulikana majina, sura wala nia yao, walivamia nyumbani kwake, Banana (uswahilini) na kumpiga risasi mtoto wa dada yake na kufariki dunia papo hapo.
MAZISHI YAKE
Marehemu Gweso amezikwa Septemba 27, mwaka huu katika Makaburi ya Kijiji cha Tailo Wilaya ya Bunda Mkoani Mara. Ameacha mke mmoja na watoto wanne.
0 comments:
Post a Comment