KITANZI KILICHO TUMIKA KUMNYONGA SADAM HUSSEIN CHAGEUKA BIASHARA

 

Kamba iliotumiwa kumyonga aliyekuwa rais wa Iraq marehemu Saddam Hussein imedaiwa kuuzwa kwa zaidi ya dola millioni 4.
Licha ya Saddam kunyongwa mwaka 2006,watu bado wanamuenzi na mtu mmoja amejitolea kulipa dola millioni 7 kununua kamba hiyo iliokatiza maisha ya kiongozi huyo wa zamani.
Kulingana na gazeti la Metro,Baadhi ya watu matajiri wanaoitaka kamba hiyo wanatoka mataifa ya Kuwait,Iran na Israel.
Dr Mowaffak al-Rubaie,mshauri wa usalama wa zamani nchini Iraq

Kamba hiyo kwa sasa inamilikiwa na Dr Mowaffak al-Rubaie,mshauri wa usalama wa zamani nchini Iraq,ambaye aliongoza eneo ambalo rais huyo wa zamani aliuawa.
Aliamua kuihifadhi kamba hiyo baadaye na sasa anataka zaidi ya dola millioni 7 kuiuza kamba hiyo.
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment