SABA YA MOYONI KUTOKA KWA MPOTO AKIWEMO RAISI KIKWETE


mboni iii

Siku ya jana February 06 kwenye Mboni Show alikuwepo Mrisho Mpoto, amepiga story na audience kuhusu vitu vingi, ikiwemo family yake, siasa na uchaguzi 2015, kilichomkuta baada ya kusikika anataka kugombea Ubunge na namna anavyomzungumzia Rais Kikwete.

Alianza kuzungumzia kuhusu familia yake; “Nina watoto wawili.. huyo mmoja ndio mtata hata simuelewi anafanya nini.. huyo mdogo ni pasua kichwa, anasema siwezi kufanya unachokifanya wewe…

Hapa alizungumzia kuhusu kwanini hasikiki kuwa na skendo; “Maisha yanatofautiana mtu kama mimi nimekuwa kama icon, watu wengi wanapenda kujifunza kupitia kwangu. Kuna matamko ya nchi.. ya Serikali napewa mimi kwa hiyo ni vizuri sana usiingie kwenye maisha ya skendo… Najaribu kukimbia skendo.

Kuhusiana na ishu ya kujitambua; “Wewe ni nani, swali la pili unatakiwa kujiuliza nani sio wewe? Swali la tatu kujiuliza ni nani unayemuamini? Mtu pekee unayetakiwa kumuamini kwenye maisha yako ni wewe

Mpoto alizungumzia pia ishu ya kukutana wagombea Urais waliotangaza nia 2015; “Mwaka huu mashabiki wangu wanisamehe tu mwaka huu nina mambo mengi sana, wote hao unaowasikia 23 nimeshaonana nao.. kuna Mrisho Mpoto halafu kuna ‘Mjomba’, kule naenda kama Mrisho Mpoto. Unatakiwa usikie mawazo yao, mimi ni sauti ya watu nasikia mawazo yao halafu nitakuja kuwaambia watu
Mboni IV
Ishu ya kilichimkuta baada ya kutangaza kugombea Ubunge; “ Hizo simu nilizopigiwa, nikasema mmmh… ni kama unanitonesha kidonda ukiniuliza maswali hayo.. nakujibu kwa mkato sitaki hilo swali

Jitihada zake kuinua utamaduni; “najaribu kushikilia muhimili wa nchi yetu, napambana sana kuhusiana na lugha

Hapa aliulizwa kuhusu anavyomzungumzia Rais Kikwete; “Kama kuna nafasi kubwa ambayo tutakuja kuikumbuka ni utawala wa huyu mtu, akija kuondoka ndio watu watakuja kukumbuka

Mboni V

Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment