Bobby Brown asema mwanawe yu hai

Imeripotiwa kuwa mashine inayomsaidia kupumua mtoto wa Whitney Houston Bobby Kristina imezimwa,hataihvyo madai hayo yamekanwa na familia yake.

Bobby Kristina amekuwa katika koma ya kimatibabu tangu apatikane nyumbani kwake akiwa uso wake upo ndani ya maji nkatika beseni la kuogea na asiye na fahamu.

Babaake Bobby Brown anadaiwa kuwa katika hospitali hiyo ya Emory University ambapo mwanawe anapata matibabu pamoja na watu wa karibu wa familia.

Imeripotiwa katika Gazeti la Mail online kwamba mashine inayomsaidia kupumua ilizimwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ,lakini familia yake imekana hilo na kusema bado msichana huyo yuko hai.

Bobby brown amesema kuwa anamuombea mwanawe na alipoulizwa alikuwa anaendeleaje, alijibu kusema kwamba yuko vyema.
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment