ASKARI wa jiji jana walilazimika kutumia mabomu ya
machozi kuwatawanya watu wanaofanya biashara kandokando mwa barabara
‘Machinga’ katika maeneo ya Tabata jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wakazi wa eneo hilo, aliyezungumza na GPL, alifafanua chanzo
cha askari kutumia nguvu hiyo, ambapo alisema ni baada ya wananchi
kuwapiga mawe wakati wakitekeleza zoezi lao.
“Majuzi askari wa jiji walikwenda maeneo ya Segerea kwa ajili ya
kufanya oparesheni ya kuwaondoa wafanya biashara kandokando mwa
barabara, wananchi wakaanza kuwapiga mawe na kufanya zoezi hilo kuwa
gumu. Ndiyo maana leo baada ya kuanza kupigwa mawe, nao wakaamua kutumia
mabomu ya machozi katika kuwatawanya.’’
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment