SITTI MTEMVU ATWAA TAJI LA MISS TANZANIA 2014

Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu katika pozi na mshindi wa pili, Lillian Kamazima (kulia) pamoja na mshindi wa tatu, Jihhan Dimachk baada ya kutangazwa mshindi.
MREMBO Sitti Mtemvu kutoka Temeke ametwaa taji la Miss Tanzania 2014 na kujinyakulia kitita cha milioni 18 usiku huu katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Nafasi ya mshindi wa pili imekwenda kwa Lilian Kamazima ambaye amejishindia shilingi milioni 6 huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Jihan Dimachk. Dorice Mollel ameshika nafasi ya nne wakati Nasreen Abdul akichukua nafasi ya tano.
Kwa ushindi huo, Sitti atapeperusha bendera ya Tanzania katika mashindano ya Miss World 2015.
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment