anasema kuwa filamu ya Tajiri Mfupi ni sinema ya kipekee kabisa kutengenezwa Bongo hivyo kila atakayenunua lazima afurahie kazi hiyo ambayo inaburudisha na kufundisha pia.
“Ukisema Ray na kazi zake hakuna asiyejua umakini wangu sasa hapa nakuja na filamu ya Tajiri mfupi sinema bora kabisa kwa mwaka huu, nimekuja kivingine natoa nafasi kwa msanii mdogo kabisa katika tasnia,”anasema Ray.
Filamu ya Tajiri mfupi imewashirikisha wasanii wakali katika tasnia ya filamu Swahilihood kama Yobnesh Yusuf ‘Batuli’, Hussein Chodo, Idrissa Makupa ‘Kupa’, Muhogo Mchungu, Ray na wasanii wengine wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu Bongo na inasambazwa na Steps Entertainment.
0 comments:
Post a Comment