MABINGWA WA DANCE 100%WAUNGANISHWA NA MTANDAO WA VODACOM


Mabingwa wa Dance 100% 2014”WAKALI SISI”wa Kiwalani jijini Dar es Salaam,wakionesha simu aina ya Vodafone Smart Kicka  zikiwa na muda wa maongezi wa shilingi laki moja mara baada ya kukabidhiwa rasmi na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu (kulia).
Meneja Uhusiano wa Umma  wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kulia) akiwakabidhi rasmi vijana wa kundi la”WAKALI SISI”la kiwalani jijini Dar es Salaam simu zao aina ya Vodafone Smart Kicka,ambazo ni moja kati ya zawadi walizojishindia  katika fainali za shindano la Dance 100% hivi karibuni na kujishindia kitita cha  Tsh Milioni 5 na simu hizo zimeunganishwa na mtandao wa Vodacom Tanzania  muda wa maongezi kiasi cha  shilingi laki moja.
Mabingwa wa shindano la Dance 100% 2014” WAKALI SISI”wakimsikiliza  kwa makini Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kulia) wakati alipokuwa akiwahusia kuhusiana na matumizi mazuri ya simu  baada ya kuwakabidhi rasmi simu zao aina ya Vodafone Smart Kicka zilizounganishwa na Vodacom na muda wa maongezi wa kiasi cha  shilingi laki moja ambazo ni moja ya zawadi walizojishindia katika fainali ya shindano hilo na kuibuka washindi wa kwanza na kujizolea kombe pamoja na kitita cha shilingi milioni 5.
 Kiongozi wa kundi la”WAKALI SISI” la Kiwalani jijini Dar es Salaam,Baraka Kambona(kushoto) akipokea mfuko wenye simu aina ya Vodafone Smart Kicka zilizounganishwa na mtandao huo na kuwekewa muda wa maogezi wa shilingi laki moja toka kwa Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu.
Kundi la”WAKALI SISI”ambalo ni mabingwa wa shindano la Dance 100% 2014 wakionesha makali yao ya kucheza dansi katika makao makuu ya Vodacom walipofika kwenye hafla fupi yakukabidhiwa  simu zao aina ya Vodafone Smart Kicka.
Na Waandishi wetu
Kundi la ”Wakali Sisi” lenye makazi yake Kiwalani jijini Dar es Salaam, ambalo liliibuka na ushindi miongoni mwa makundi matano yaliyoingia fainali za shindano la kucheza muziki maarufu kama Dance 100% na kujishindia kitita cha shilingi milioni 5 wiki iliyopita leo/ jana  wasanii wa kikundi hicho walikabidhiwa simu aina ya smart Phone na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom.
Akiongea katika hafla ya kuwakabidhi zawadi ya simu Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu,alisema kuwa kwa kushinda mashindano hayo wamedhihirisha kuwa wana kipaji kikubwa na aliwataka wasibweteke bali wajiendeleze ili waweze kupata mafanikio zaidi.
“Vodacom tunaamini kuwa sanaa na michezo inaweza kutoa ajira kwa vijana ndio maana  tumekuwa tukidhamini michezo na sanaa hivyo tumia vizuri pesa mlizopata na  simu hizi tulizowazawadia kutafuta fursa za kusonga mbele na kupata mafanikio zaidi nasi tutazidi kuwaunga mkono”Alisema Nkurlu.
Naye msemaji wa kundi hilo Baraka Kambona  aliishukuru kampuni hiyo kwa zawadi hizo za simu  na kuongeza kuwa mashindano hayo yamewafumbua macho  na wameweza kujulikana na kuahidi kuendelea na mazoezi na ubunifu zaidi ili kundi lao lizidi kutamba katika ushindani mkubwa wa sanaa ya muziki kwani hata jana tulitumbuiza kwenye shindano la Miss Tanzania.
Shindano hilo linaloratibiwa na Kituo cha East Africa Television na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania, lilikuwa la kukata na shoka kwa ushindani mkali na lilifikia tamati Oktoba nne katika Viwanja vya Don Bosco, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Makundi matatu yalifanikiwa kujinyakulia zawadi mbalimbali katika hatua ya fainali hiyo na vijana walikuwa wakionesha vipaji na umahiri mkubwa wa kucheza staili mbalimbali za muziki ambayo ni Wakali sisi walioibuka kidedea na kujinyakulia kitita cha Sh5 Milioni huku kila mshiriki katika katika kundi hilo akipatiwa simu aina ya Vodafone Smart Kick ikiwa na muda wa maongezi wa Sh 100,000.
Mshindi wa pili ni kundi la The W.T. ambalo lilijinyakulia Sh1.5 Milioni na mshindi wa tatu ni kundi la Wazawa Crew lilijinyakulia Sh500,000.
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment