
MSANII wa Bongo Fleva, Ali Kiba usiku wa kuamkia leo akiwa nyumbani kwake Kunduchi jijini Dar es Salaam, alivamiwa na kundi la watu wapatao 20 wanaodhaniwa kuwa ni majambazi.

Nyumbani kwa Ali Kiba Kunduchi jijini Dar es Salaam baada ya kuvamiwa.
Ikiwa utakuwa na taarifa zozote zitakazosaidia kupatikana kwa majambazi hao, unaweza kutoa taarifa katika kituo cha polisi ulicho karibu nacho.
Abdu Kiba, amesema yeye alikuwa Masaki, Ali akampigia simu kwamba kuna watu kama 15 hivi wamevamia nyumbani kwao.. waliovamia waliruka ukuta saa tisa usiku, wakavunja mlango wa sebuleni, wakakuta vijana wawili ambao wanaishi nao, wakawapiga na kuwalazimisha wawaoneshe chumba ambacho Ali yumo.. wale vijana wakajibu kwamba Ali hayupo, wakaulizia chumba chake wakaoneshwa chumba cha Abdu Kiba.
Wameingia chumbani wakamkosa Ali Kiba, wameiba vitu vingi vya sebuleni na chumbani pia, pamoja na pesa milioni 2 na nusu zilizokuwa chumbani kwa Abdu.
Abdu amesema alitoa taarifa Polisi, wakafika usiku huo huo na kuanza ukaguzi wa eneo lote la nyumba.
Wakati tukio lote linaendelea Ali alikuwa ndani kwenye chumba kingine, hawakuomuona.
Wale vijana wawili waliokutwa sebuleni wameumizwa kutokana na kupigwa,
wametibiwa na kurudi nyumbani.. silaha walizoingia nazo hawajajua ila
liko jiwe zito na chuma kizito ambacho kilitumiwa kuvunja milango wakati
wanaingia.
Mlango wa chumbani kwa dada yake Ali Kiba umevunjwa kabisa.
0 comments:
Post a Comment