Mkurugenzi wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Said Fella amempa zawadi ya
gari kiongozi wa Yamoto Band Aslay Isihaka ambaye jana (May 7) alikuwa
akisheherekea siku yake ya kuzaliwa.
Fella akimkabidhi Aslay fungua za gari aliyomzawadia
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Fella alipost picha alipokuwa akimkabishi gari hiyo na kuandika ujumbe mrefu wa kumpongeza.
“MUNGU NDIO KILA KITU TATIZO MUDA NA SUBRA INSHAALLAH MWANETU ASLAY
KITUO CHETU CHA MKUBWA NA WANAWE YOUTH CENTRE TEMEKE MIKOROSHINI TUNAJUA
MCHANGO WAKO TANGU TUANZISHE KITUO IKI LEO TUMEONA WACHA TUKUZAWADIE
NYEZO ILI MURADI IWE CHANGAMOTO KWA WENZAKO KITUONI APA KUONGEZA BIDII
NA UPENDO NA KUJITOA KUSAIDIA WENZAO KAMA ULIVYO JITOA WEWE KWA WENZAKO
INSHAALLAH MUNGU TUBARIKI SOTE SIE NA WADAU WETU PIA ATULINDIE AMANI
YETU.baadaye tukutane matei jijini dodoma kwa burudani ya mkubwa na
wanawe ya moto band njoo tucheze ngoma ya vijana mpya kimadoido.”
Aslay naye alipost picha hiyo na ujumbe mrefu wa shukrani.
“Asante mungu Kwa kunipa uhai Na kipaji ambacho leo hii kina fanya
naitwa Aslay pia nakushukuru kwa kunifikisha kwenye mikono Ya mtu mwenye
moyo wa kibinaadamu. Najua kuna mengi makubwa ambayo boss wangu
@mkubwafella umenifanyia ambayo si vyema kuyataja yote kwasababu wakati
wake haujafikia ila naomba nichukue fulsa hii kukushukuru kwa hiki
ulichonifanyia leo katika sherehe Ya kusherehekea siku yangu Ya kuzaliwa
umenifanya nijione mwenye thamani kubwa duniani sikutegemea kama leo
itakuwa siku yangu ya kumbukumbu ambayo sitoweza kuisahau hata Nije kuwa
bilionea @mkubwafella asante kwa kunipa hii zawadi ambayo mimi kama
mimi sikuiwazia kabisa kama Leo nitapata gari Na ninaushukuru uwongozi
mziki Wa #mkubwanawanawe pamoja na manager wangu @chambusso boss wangu
@babutale @mhtemba na mama yangu @sweatfella bila kuwasahau wasanii
wenzangu wa @yamoto_band mungu ndie atakaewalipa … Nawatakia usiku mwema
woote na Watu wa Dodoma Tukutane kesho pale Matei.”
ASLAY APOKEA ZAWADI YA GARI KUTOKA KWA MANAGER WAKE
08 May
Bongo yetu
,
isikupite
,
Ma Star wetu
,
Photo
,
Utaipenda
0 comments:
Post a Comment