Kutoka kwenye performance ya wimbo wake ‘Ni Penzi’ iliyompa kura chache wiki iliyotangulia, wiki hii Damian alithibitisha uwezo wake wa kubadilika baada ya kuimba wimbo wa mwalimu wa washiriki wa Maisha Superstar, Erick Wainaina ‘Nchi ya Kitu Kidogo’
Kilichomfanya atishe zaidi ni kubadilisha wimbo huo kuwa sebene na kurap kama wafanyavyo waimbaji wa bendi za dansi. Damian ndiye aliyepata kura nyingi zaidi wiki hii.
Naye mshiriki mwingine wa Tanzania, Myra ambaye mentor wake ni Shaa, alifanya vizuri pia kwa kufanya mash-up ya nyimbo za Beyonce Drunk in Love na Diva.
0 comments:
Post a Comment