Rapper Fareed Kubanda aka Fid Q amedai kuwa kampeni aliyoanzisha
mwaka jana ya Tu8 January ambayo ilishuhudia kufanyika kwa ziara za
wasanii katika baadhi ya maeneo nchini, haina uhusiano wowote na January
Makamba.
Akiongea kwenye kipindi cha Mambo Mseto cha Radio Citizen ya Kenya,
Fid alisema kampeni hiyo ilijihusisha na kuwataka vijana kujitokeza
kwenda kujiandikisha kupiga kura na kujitokeza kwaajili ya kugombea
nafasi za uongozi.
“Ni kwasababu Tanzania tulipofanya sensa juzi kati hapa ikaonekana
kabisa kwamba 80 percent ya watanzania ni vijana. Kwahiyo huwa tuna
msemo wetu vijana ni taifa la kesho lakini sasa umekuwa sio tena taifa
la kesho, ni taifa la sasa so the future is now,” alisema.
“Nani wa kuweza kutusaidia sisi the majority? Ni vijana wenzetu ambao
wanajua matatizo yetu, so my idea ni kwenda kuwaamsha vijana.”
Msikilize hapo chini.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment