Watu 10 wakiwemo wanamichezo wa olimpiki wa Ufaransa walioshindana
kwenye mashindano hayo ya London 2012 wamekufa baada ya helikopta mbili
kugongana hewani nchini Argentina jana. Watu hao walikuwa kwenye
mchakato wa kutengeza kipindi cha TV.
Washindi wa Olimpiki Camille Muffat, katikati, Florence Arthaud,
wa pili kutoka kulia na Alexis Vastine wa mwisho kulia wakiwa pamoja na
washiriki wenzao wakiwa njia kwenda kushoot kipindi cha reality cha
‘Dropped’. Mchezaji wa zamani wa Arsenal, Sylvain Wiltord (katikatia
kushoto) alikuwa kwenye show hiyo lakini hakuwa amependa kwenye
helikopta hizo
Camille Muffat, 25, mwogeleaji aliyeshinda midani ya dhahabu kwenye
shindano la wanawake la 400m freestyle mwaka 2012, bondia wa olimpiki,
Alexis Vastine, 28, aliyeshinda midani ya fedha kwenye mashindano hayo
yaliyofanyika Beijing, 2008 ni miongoni mwa waliopoteza maisha.
Waliopoteza maisha ni pamoja na marubani wawili wa Argentina na raia
wengine watano wa Ufaransa waliokuwa wakishiriki kwenye kipindi
kiitwacho Dropped.
Mamlaka zimesema hadi sasa haijulikani chanzo cha ajali hiyo
iliyotokea magharibi mwa jimbo la La Rioja jirani la milima ya Andes.
Home / isikupite /
News
/ Watu 10 wapoteza maisha baada ya helikopta mbili kugongana hewani wakati wakishoot reality show
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment