Tumesikia story nyingi kwenye vyombo vya
habari vya Kimataifa, nyingi zaidi utasikia kwenye ishu kama kama
ubadhirifu, matumizi mabaya ya madaraka, rushwa na mengine, ni mara
chache kukutana na stori za viongozi wakizungumziwa kwa mazuri.
Rais wa Namibia anayemaliza muda wake, Hifikepunye Pohamba ameshinda tuzo yenye thamani kubwa ya Mo Ibrahim inayotolewa kwa viongozi wa bara la Afrika.
Tuzo hiyo hutolewa kila mwaka kwa
kiongozi wa nchi ambaye ameshika madaraka kwa kuchaguliwa na wananchi na
aliyeongoza vizuri nchi yake pamoja na kuboresha maisha ya wananchi
akiwa madarakani.
Rais Pohamba anakaribia kumaliza muda wake wa kuiongoza Namibia kwa awamu mbili.
Mfanyabiashara raia wa Sudan, Mo Ibrahim ndiye mwanzilishi wa Tuzo hiyo na aliianzisha kwa ajili ya kuwapa motisha viongozi wa Afrika.
Zawadi ya dola mil. tano inatolewa kwa
kipindi cha miaka kumi kwa mshindi wa Tuzo hiyo, halafu baada ya hapo
atakuwa anapewa dola laki 2 kila mwaka mpaka mwisho wa maisha yake.
0 comments:
Post a Comment