Mwandishi filamu za Jacob ‘JB’ Stephen, Daniel Manege amemtetea
muigizaji huyo kuwa hakuwa na makosa ya kuigiza filamu ya ‘Mzee wa
Swagga’ ambayo ni kopi ya filamu ya kihindi, Ladies Vs Ricky Bahl.
Manege aliyeiandika filamu hiyo pamoja na zingine zikiwemo Dereva
Taxi, Nakwenda kwa Mwanangu, Shikamoo Mzee, Bado Natafuta zingine,
ameandika ujumbe kupitia Facebook na kudai kuwa JB si mtu wa kulaumiwa
bali ni yeye mwandishi.
“Kwanza kabisa ningeanza kwa salam kwenu nyote na naamini muwazima wa
afya. Nimeamua kuandika ujumbe huu baada ya kuona na kupigiwa simu
chache kuhusu uvumi wa filamu Mzee wa Swagga kuwa imekopiwa. Nijibu jibu
fupi bila kusita kuwa kweli Story imekopiwa na original Story inaitwa
Ladies Vs Ricky Bahl na mimi ndiye niliyemshauri JB kuichukua Story hiyo
yenye maudhui ya kuvutia,” ameandika.
“Nataka nieleze sababu ya kufanya hivyo ila kabla sijaeleza sababu
ningependa kuwaambia wale wote wanaotumia skendo hii kuyarefusha mambo
haya kuwa kwenye ulimwengu wa filamu ni jambo la kawaida duniani watu
kuchukua maudhui ya story na kuyatengeneza katika mazingira yao endapo
maudhui hayo yataelimisha au kukosoa au kufurahisha kuhusu
jambo..watakaoendelea kulalamika baada ya ujumbe huu ni dhahiri wanania
zao nyingine na si kujenga.”
Kwanza kabisa mimi ndiye mwandishi mkubwa wa filamu za JB kuanzia
enzi za DJ Ben, Dereva Taxi, Nakwenda kwa Mwanangu, Shikamoo Mzee, Bado
Natafuta mpaka hii Mzee wa Swagga na hizo nyingine zote zikiwa ni
original scripts kutoka kwenye ubongo wangu. Filamu anazofanya JB ni
Romantic Comedies na Inspirational Comedies kwa hiyo yeye huwa anapenda
maudhui ya kuentertain zaidi yani filamu zenye kuchangamsha na
kuburudisha tofauti na waigizaji wengine kama Single Mtambalike
anayependelea filamu za ugentleman zaidi (haya ni kutokana na kukaa nao
na kuzungumza nao na kuwafahamu kwa kina)
Sasa kuhusu Mzee wa Swagga, JB alitengeneza filamu mfululizo zenye
maudhui tofauti na alizozoeleka, kama Hukumu ya Ndoa, Mikono Salama
ambazo sikuziandika mimi na nakiri kuwa hazikufanya vizuri sana sokoni.
Sababu ya filamu hizi kuandikwa na watu wengine ni sababu nilikuwa
nashughulika na Script ya filamu yangu mwenyewe niliyoproduce mwaka jana
October inayoitwa SAFARI YA GWALU (bado haijatoka mpaka mwezi wa 3
mwishoni), aliyoigiza Gabo kama kijana anayerudi shule ya msingi baada
ya kupigika na maisha.
Filamu hii imenichukua mwaka mzima kuanzia kuiandika mpaka kuja
kuproduce, kuandika ilianza January-march 2014 hivyo sikupata nafasi
kumuandikia JB tangu tulipotoa BADO NATAFUTA na CHARLE MVUVI (bado
haijatoka). Baada ya filamu hizi mbili (Hukumu ya Ndoa na Mikono Salama)
JB alinieleza angetamani nimuandalie Filamu na Mzee Majuto wakati huo
wakiwa safarini kwenda Uturuki ili wakashoot Uturuki iwe filamu kali.
Wakati nikiandaa filamu hiyo mshtuko mkubwa ukaja kwa misiba ya
mfululizo ya wana Tasnia wenzetu iliyopelekea Safari ya JB na Mzee
Majuto ya Uturuki kufa na hivyo kufanya hata script niliyoandaa kukosa
msisimko tena.
Baada ya matatizo JB alitaka filamu inayofanana na Senior Bachelor,
DJ Ben na Nakwenda kwa Mwanangu, akiigiza kama mburudishaji zaidi na kwa
kuwa sikuwa na Idea mpya kwenye kichwa na muda ulikuwa unaenda sana na
anahitajika kupeleka filamu yake kwa msambazaji ikabidi nitafute story
itakayofanana na JB mburudishaji tunayemfahamu muda mrefu, kwa kuwa mimi
ni gwiji wa filamu haikuwa ngumu kutafuta na ndipo tukaipata Ladies Vs
Rick Bahl, JB aliipenda ila sote tulikuwa na wasiwasi kwani JB ni muoga
sana wa kuandikwa vibaya, nikamwambia jambo ambalo nataka niwaeleze
nanyi leo. Jambo ambalo lilimfanya JB kukubali niandike script mpya
kupitia kisa kile na kuiproduce..
Ukweli ni kuwa duniani kote watu wanapoona maudhui ya story ya nchi
au taifa jingine kuwavutia wanaweza kuchukua maudhui hayo na kuyatumia
kutengeneza filamu za maudhui yale kwenye mazingira yao. Kuna Filamu
nyingi hapa Tanzania na Nigeria na Bollywood Hata Hollywood zimefanyika
hivyo na si dhambi. Kama Tanzania tazama filamu Ya BEST MAN ya Hemedi na
Yussuf Mlela, ni copy ya BEST MAN ya Morris Chestnut na Taye Diggs…
Nollywood filamu Ya GUARDIAN ANGEL ya Ramsey Noah ni copy ya Filamu
HATYA ya Bollywood ya Govindah…Pia filamu za ROMEO AND JULIET developed
kutoka kwa William Shakespears plays zimekopiwa Bollywood kwenye filamu
iliyoleta Mabadiliko makubwa Bollywood ya QAYAMAT SE QAYAMAT TAK kama
nasema uongo mtu aziangalie na kuja kunikosoa na nitaleta dazeni ya
filamu zilizokopiwa kutoka nchi na nchi. Ila nataka kuuliza swali mbona
nyingine zilizokopiwa hapa Tanzania toka nje hazikuzungumziwa kama Mzee
wa Swagga? Nadhani jibu ni sababu JB ameitendea haki filamu hiyo, ila
tusiende huko
Jambo jingine, mnapokaa kulaumu mjue kazi ya kuwapa watazamaji kitu
wanachotaka kila siku na kuwafanya wakupende si suala dogo, tunaumiza
vichwa mchana na usiku. JB si kwamba namfagilia sababu namuandikia ila
huwa anaumia sana kutafuta story mpya na ukweli hata mimi nateseka sana
kutengeneza vitu vipya na ukitazama mtu huyu mmoja atengeneze filamu 6
au 7 kwa mwaka na zote mzipende na kufurahia inahitaji kujitoa kwa hali
ya juu. Nikiwa kama mwandishi kihalali nahitaji kuandika script 2 tu kwa
mwaka ili nitoe vitu vikali, unapoelemewa na mzigo ni rahisi kuharibu
kazi na kwa kuwa tunajitahidi (mimi na JB) kuwapa mnachopenda basi huwa
tunatafuta kila njia kutowakwaza mashabiki, naomba mtuhurumie nasi kwani
mazingira ya kazi ni magumu mno.
Kwa haya niliyoandika ningependa kuwaambia tusiwe watu wa kulaumu na
kuhukumu, mimi kuproduce filamu yangu mwaka jana kumepunguza kujitoa
kwangu kuandaa filamu kali za JB, mimi ndiye wa kulaumiwa na si JB. Na
kwa niaba ya mashabiki wa JB nawaomba radhi kama kwa namna moja au
nyingine mmejisikia vibaya ila kwa niliyoeleza mtaungana nami kuwa si
dhambi kufanya hivyo inapobidi na tushirikiane kupeleka gurudumu hili
mbele. Mimi ndiye mwandishi bora wa script na natambua jukumu langu kama
mwandishi simkingii kifua JB bali nasimamia kile ninachokifanya kama
Professional. Naomba tuache kuongea na tushirikiane kuboresha filamu
zetu.”
Home / Bongo Movie /
Bongo yetu /
Elimu ya Bongo /
Entertainments /
Utaipenda
/ Ni kweli nimekopi filamu ya kihindi – mwandishi wa filamu mpya ya JB
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment