MASTAA wanane wa Yanga ambao wengi wao wanacheza katika kikosi
cha kwanza, wamebakiza miezi mitatu tu katika mikataba yao ya sasa na
watakuwa huru mwishoni mwa msimu, Mwanaspoti imebaini.
Hata hivyo, uongozi wa klabu hiyo licha ya
kutotaja majina ya mastaa hao, umesisitiza kwamba watapambana kiume
kuhakikisha hakuna yeyote atakayechoropoka klabuni hapo.
Katibu wa Yanga, Jonas Tiboroha alikiri mastaa hao
wanaelekea ukingoni mwa mikataba yao na kudai klabu hiyo ilifanya
makosa kuchelewa kuwaandalia mikataba mipya, lakini ametoa ahadi nzuri
kwa wapenzi wa klabu hiyo kuwa hakuna mchezaji muhimu atakayeondoka
mwishoni mwa msimu kama ilivyotokea msimu uliopita.
“Ni kweli tuna wachezaji kama wanane ambao
mikataba yao imebakiza miezi michache, itamalizika mwishoni mwa msimu,
kuna makosa kidogo yalifanyika kukubali mikataba ya wachezaji wengi
kufikia ukingoni kwa pamoja,” alisema Tiboroha ambaye ni msomi wa ngazi
ya PHD.
“Kuna wachezaji ambao ni muhimu sana na mikataba
yao nayo inakwisha, lakini hawataweza kuondoka kama ilivyokuwa kwa kina
Frank Domayo na Didier Kavumbagu, tumeanza kazi ya kuangalia wale
tunaowahitaji ili tuwapatie mikataba mipya.”
Katibu huyo ambaye ni mkufunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) aligoma kuweka wazi majina ya mastaa hao.
“Siwezi kusema ni nani na nani ambao mikataba yao
inakwisha, itakuwa rahisi kwa wapinzani wetu kuwapata, kikubwa ni kwamba
wote tunaowahitaji tutawaongezea mikataba na pia tutaanza mazungumzo na
wale waliobakisha mwaka mmoja ili kuwaongeza, hatutaki tena wachezaji
wengi wacheze wakiwa na mikataba ya miezi michache,” alisema Tiboroha.
“Katika hilo wanachana na mashabiki wetu waondoe wasiwasi kila kitu kitawekwa sawa.”
Hata hivyo, Mwanaspoti linafahamu kuwa miongoni
mwa wachezaji hao ni kipa Deo Munishi ‘Dida’, beki Mbuyu Twite, Kiungo
Haruna Niyonzima, Nizar Khalfan na mshambuliaji Mrisho Ngassa.
Tayari mkataba wa Dida upo umeshaandaliwa lakini
bado haujasainiwa na mazungumzo bado yanaendelea kwa Haruna na Twite
ambao wanahitaji kubadilishiwa masilahi na dau la usajili ingawa habari
za ndani zinadai kwamba wachezaji hao wanataka kupewa dau lote kwa
mujibu wa makubaliano.
AIZUNGUMZIA
MECHI YA BDF
0 comments:
Post a Comment