Kumekuwa na matukio mengi yanayotokea ndani ya Mabunge mbalimbali duniani halafu yanachukua headlines kubwa mtaani na mitandaoni, tumeona ya TZ, Kenya, Afrika Kusini ile juzi wakati Rais Zuma akiwa anahutubia, hii nakupa na wewe uipate kutoka ndani ya Mjengo wa Bunge Canada.
Mbunge Pat Martin naye katoa kali ya mwaka, ile story yake aliyoitoa yani hakuna Mbunge ambaye hakucheka.
Kulikuwa na ishu ya kupiga kura
ikiendelea ndani ya Bunge hilo, Mbunge huyo akahojiwa sababu iliyomfanya
awe nje ya Jengo wakati zoezi la kura likiendelea, katika kujitetea
akajibu kwamba alijikuta akilazimika kutoka nje ya kikao kutokana na
nguo ya ndani aliyokuwa ameivaa ilikuwa ikimbana sana hivyo asingeweza
kuvumilia kuendelea kukaa ndani ya kikao hicho.
Pat Martin alijitetea
kwamba anadhani kilichomponza ni kitu ambacho kimewaponza wengi pia
ishu ya kutaka kununua vitu vya bei poa ama kuomba kupunguziwa bei za
vitu.
Yeye alinunua nguo hizo za ndani nyingi
baada ya kuzikuta zikiuzwa kwa nusu bei, akanunua nyingi bila hata kujua
kama zilikuwa zinamtosha size au hapana.
0 comments:
Post a Comment