a
Lupita Nyong'o akiwa amevalia vazi linalotajwa kuwa na gharama kubwa
Nguo iliyobuniwa na kampuni ya
Calvin Klein yenye thamani ya dola 150,000, na kuvaliwa na msanii
maarufu wa kike Lupita Nyong'o katika tuzo za Oscar imeibiwa Hollywood .
Gauni
hilo lililobuniwa kwa namna ya pekee na kupambwa kiasilia na konokono
weupe zaidi ya 6,000 toka baharini, lilichukuliwa kwenye hoteliya London
magharibi mwa Hollywood.
Lupita Nyong'o kutoka nchini Kenya
aliibuka msanii bora wa kike mwaka jana baada ya miaka kumi na mbili ya
utumwa, Lupita alikuwa mtangazaji wa sherehe za jumapili.
Baadhi ya magazeti yanamwita Lupita Nyong'o mrembo wa mwaka 2014.
Sheriff
William Nash anasema nguo hiyo inaonekana kuibiwa siku ya jumatano
jioni na polisi wanaendelea kufanya uchunguzi kupitia kamera maalum za
CCTV.
0 comments:
Post a Comment