Tunda Man anatarajia kwenda Muscat, Oman au Dubai kwenda kushoot video ya wimbo wake ‘Achana na Mimi.’
Akizungumza na Bongo5 hivi karibuni, Tunda alisema ameamua kwenda
Dubai kutokana na aina ya mazingira ambayo video yake inayahitaji.
“Nimepokea maoni ya video ya Achana na mimi kwahiyo nawa-promise
kwamba nitafanya kwasababu nataka nikafanye Muscat au Dubai kwahiyo
nilikuwa naangalia process za kwenda kule zinakuwaje,” amesema muimbaji
huyo.
“Ndo mchakato ambao ninao sasa hivi nataka niushughulikie sasa hivi
ili ikiwezekana mpaka mwezi wa tatu kazi iwe imeshatoka. Nimeamua kwenda
kufanya Dubai kwa sababu wimbo wenyewe unahitaji mandhari ya nchi za
kiarabu hata ukiangalia beat ipo kama kiarabu fulani hivi,” ameongeza.
Tunda Man amedai kuwa bajeti ya kukamilisha video hiyo ni zaidi ya shilingi milioni 14.
Katika hatua nyingine Tunda Man ameshare picha ambazo hajaeleza ni za nini japo zina dalili za kuwa ni video.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment