Izzo Bizness aeleza utofauti wa ngoma yake na Shaa ‘Kidawa’

Rapper kutoka Green City Mbeya, Izzo Bizness, anatarajia kuachia ngoma yake ya kwanza kwa mwaka huu. Izzo amesema ngoma hiyo iitwayo ‘Kidawa itawagusa wengi na pia kubadili mahusiano mengi ya kimapenzi.
10995270_491148947691026_222357736_n
Akiongea na E-News ya EATV, Izzo alisema:
Hii inakuwa rekodi ya kwanza kwangu kusimamiwa chorus na nyota wa kike ambaye ni Shaa. Halafu unajua jina la Kidawa ni majina ya watoto wa kike ambao wamezoeleka huko uswahilini. Huwezi kukuta mtoto anaitwa jina hilo Masaki, Mikocheni,Oysterbay. Sasa humu nimeelezea kuwa hili jina la Kidawa unaweza kulinyambulisha tofauti na watu walivyozoea. Hii unaweza kumueleza hata mtu wako wa karibu kupitia jina la Kidawa. Kwahiyo mashabiki wakae tayari kusikia hiyo ngoma.”
Hivi karibuni kupitia Instagram, Izzo aliandika: Naomba mnisikilize vizuri na Naomba mninukuu hii kauli yangu “Baada ya video hii ya KIDAWA kutoka Asilimia 98% ya wanawake waliopo kwenye Mahusiano(mapenzi) watabadili majina yao na kujiita wakina KIDAWA au a.k.a zao zitakuwa KIDAWA…..Fanya kumtag yoyote ambaye yupo kwenye mahusiano ajionee ili. KIDAWA VIDEO COMING SOON.
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment