Cristiano Ronaldo, Irina Shayksasa basiii..!

Mchezaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameachana na mpenzi wake raia wa Urusi, Irina Shayk.
LFP Awards Gala 2014
Wawili hao wamedumu kwa kipindi cha miaka mitano.
“Tunathibitisha kuwa Irina Shayk amevunja uhusiano wake na Cristiano Ronaldo,” mwakilishi wake aliiambia Page Six jana.
article-2524687-1A24ECB100000578-327_634x529
Tetesi za kuachana kwa mastaa hao zilianza kuvuma baada ya Shayk kutoonekana akiwa na Ronaldo kwenye tuzo FIFA Ballon d’Or jijini Zurich Jumatatu.
Badala yake mchezaji huyo alisindikizwa na mama yake, Maria Dolores dos Santos Aveiro, na mwanae Cristiano Jr aliyezaa na mwanamke asiyejulikana.
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment