TFF: YATOA ONYO KALI KWA TIMU ZINAZO TEGEMEA USHIRIKINA


Wakati dunia ya sasa katika soccer ikiamini kuwa ni mchezo wa kisayansi,unaotumia akili nyingi na nguvu kidogo, lakini bado dhana hiyo ni tofauti katika nchi kadha duniani na hasa barani Afrika.

Vitendo vingi zimekuwa vikishuhudiwa vikiashiria uchawi au ushirikina katika soka kitendo ambacho kinalaaniwa kwa kurudisha nyuma maendeleo ya mchezo huo maarufu duniani.

Kutokana na hilo, Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania (TFF) limesema vitendo vinavyoashiria ushirikina havitavumiliwa katika ligi kuu na timu zitaendelea kuhukumiwa kwa mujibu wa kanuni.

Mkurugenzi wa mashindano wa TFF, Boniface Wambura amesema baadhi ya timu zimeadhibiwa kwa kuamini Imani za kishirikina katika jitihada za kutafuta ushindi.

“Tumeshuhudia mara kadhaa kuona mchezaji, kiongozi au shabiki akifukia kitu uwanjani au sehemu ya goli kabla ya mechi “.

“Wengine wakirusha ndege (njiwa) na baadhi ya timu zikigoma kutumia mlango wa kuingilia uwanjani au kugoma kuingia katika vyumba vya wachezaji kwa dhana potofu kuwa patakuwa na uchawi”, amesema Wambura.

‘Wakati mwingine, si vilabu, ni mashabiki, lakini kwa kufuata nembo za jezi zao, tunatoa adhabu”, alisema
Kwa mujibu wa kiongozi huyo, kanuni za ligi zinatoa adhabu ya Sh500,000 (wastani wa dola 280) kwa kosa au kitendo kinachoashiria ushirikina.

“Kinachofanyika, wakati mwingine sio ushirikina, ila kwa kuwa kuna watu ndio kazi yao, inabidi wafanye ili kuwaogopesha wachezaji wa timu pinzani kisaikolojia, lakini kwetu ni kosa pia”.

Alisema kuna timu hivi karibuni iligoma kuingia chumba cha wachezaji na ilifanikiwa kushinda mechi na toka hapo timu nyingi zimekuwa na Imani hiyo.
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment