USHINDI WA PILI KWA SIMBA BAADA YA DROO NA KICHAPO KWA MDA MREFU




Mabingwa wa zamani wa Tanzania Bara, Simba Sports Club wamefanikiwa kuuona mwezi baada ya Mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Dan Sserunkuma kufunga magoli mawili na kuiwezesha kuifunga timu ngumu ya JKT Ruvu 2-1 katika mchezo wa ligi kuu ya soka uliofanyika Dar es Salaam.
 Mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Dan Sserunkuma


Huo ni ushindi wa pili kwa Simba baada ya bundi kuinyemelea na kupata droo zaidi ya nane mfululizo tangu ligi ilipoanza. Bao la JKT Ruvu lilifungwa na George Minja.
Kusuasua kwa Simba katika ligi kumepeleka kufukuza makocha wawili wa kigeni akiwemo Mzambia Patrick Phiri, aliyetupiwa virago hivi karibuni.

Bundi mara ya mwisho aliweka kambi klabuni hapoi baada ya Simba kufungwa 2-1 na timu ya Mbeya City siku kadhaa zilizopita na kupelekea taarifa kutoka vyombo vya habari kuwa kocha msaidizi na mchezaji wa zamani kujiuzulu kwa kile alichoeleza kuwa ni mambo ya kifamilia.

Ushindi huo unaifanya Simba kuwa ya tano katika msimamo wa ligi ya timu 14 ikiwa na pointi 16 baada ya mechi 12 na kujinasua kutoka mkiani
. Ligi hiyo inaongozwa na mabingwa watetezi, Azam wakiwa na alama (points) 21, Yanga (18), JKT Ruvu( 18), Mtibwa Sugar 17 na Simba 16.
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment