Tanzania yaifunga Nigeria


 Kriketi:Tanzania yaifunga Nigeria

Baada ya kufungwa na Kenya, timu ya Tanzania imeibuka na kuifunga Nigeria kwa wiketi tatu katika mwendelezo wa michuano ya kufuzu kucheza kombe la Dunia kwa kwa wavulana chini ya miaka 19 inayoendelea Dar es Salaam.
Mechi hiyo ilifanyika Katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam huku Nigeria wakipata nafasi ya ku-tosi na kupata mikimbio 105
Wenyeji walifanikiwa kupata mikimbio 108 na kupoteza wiketi 7 katika zamu yao huku Salum Jumbe akipata mikimbio 45 katika mipira 64 aliyopiga. Kwa upande wa Nigeria, Akachukwu Chima alifanikiwa kupata mikimbio 22 katika mipira 50 aliyopiga.
Matumaini ya wenyeji Tanzania kufuzu yaliingia doa baada ya kufungwa kwa Kenya kwa runs 11 katika mechi nzuri ya kuvutia ya kufuzu iliyochezwa katika uwanja wa Gymkhana Dar es Salaam.
Hiyo ilikuwa ni mechi ya pili kwa wenyeji kupoteza, hivyo kutoa nafasi kwa Namibia, iliyoshinda mechi zote nne, baada ya kuwafunga Uganda kwa runs 39 katika mechi iliyofanyika Gymkhana Club.
Botswana pia iliwafunga Kenya kwa mikimbio 10 katika mechi iliyochezwa uwanja wa Annadil Burhani.
Michuano hiyo inaisha Alhamis na Namibia ikiwa na pointi 8 baada ya kushinda mechi zote, ikiwa katika nafasi nzuri ya kufuzu kucheza Kombe la Dunia, kutegemea na matokeo ya mechi za leo.
Wenyeji Tanzania , Kenya na Uganda (zote zikiwa na pointi 4 kila moja) pia zina nafasi ya kufuzu na kugombania nafasi ya pili ili kucheza katika michuano ya mwisho ya kufuzu itakayofanyika Bangladesh kwa ajili ya kutafuta tiketi ya mwisho, endapo Namibia itafuzu..
Nigeria na Botswana zina nafasi finyu baada ya kila moja kuwa na pointi 2 katika michezo mine iliyocheza (kila moja).
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment