SELFIE kutumika hadi ma ofisini tena yaanzia BENKI

Lloyd IISELFIE ni kama ndio neno la mjini hivi, watu na simu zao basi ni full kujiachia, wanapiga selfie zao halafu wanashare Instagram na watu wao basi inakua poa tu yani.
Unajua teknolojia inarahisisha maisha kila siku, sikuwahi kufikiria kwamba kuna siku hizi selfie zitachukua nafasi ya passport size!
Mara  nyingi tunazitumia passport size kwenye vitambulisho vyetu au cheti hivi au sehemu yoyote inapotakiwa, nakusogezea hii kutoka Uingereza ambako Benki ya Lloyds imeanzisha utaratibu huu, kama unataka kufungua account huna haja ya kupiga passport size, selfie yako moja tu basi kazi imeisha.Lloyd
Mteja atakachotakiwa kufanya ni kupiga selfie yake moja na pia kupiga picha ya passport iliyo kwenye leseni, au kitambulisho chochote halafu anatuma, kompyuta ikitambua tu kwamba picha hizo mbili ni za mtu mmoja basi mteja anaendelea zake na taratibu nyingine kufungua account mpaka inapokamilika.
Tunajua kwamba watu wako busy na majukumu ya kimaisha duniani kote, Uingereza wameifurahia hii, wanasema ni rahisi na itaokoa sana muda wao kukamilisha kila kitu mtandaoni wakati wa kufungua account.
Natamani niione hii Bongo siku moja, hapo vipi mtu wangu?
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment