Unaweza kujiuliza mara mbilimbili inakuaje mpaka mtu anapata ujasiri wa kumuuza mama yake mdogo? tena aliekamilika?
1.
Mwanamke mwenyewe alieamua kumuuza mama yake mdogo, anaitwa Sophia Yasin
Chambo (30) na ilikua February 17 2015 saa nane mchana maeneo ya
Lizaboni, alikwenda nyumbani kwa Mfanyabiashara wa eneo hilo na
kumwambia anahitaji kufanya nae biashara ili azidi kuwa tajiri.
2.
Alimwambia anae mama yake mdogo na angehitaji kumuuza kwake ili amfanye
kama zindiko biashara izidi kumuingizia pesa, alikubaliana kwamba
atampeleka Mama mdogo akiwa kwenye gunia baada ya kumuua lakini
Mfanyabiashara akasema anamtaka akiwa hai.
3.
Walikubaliana bei ni Milioni 6.5 kutokea kwenye Milioni 10 aliyoanzia,
kesho yake kweli Sophia alikwenda kumchukua mama yake mdogo aitwae Anita
Kasim Mbawala mwenye umri wa miaka 40.
4.
Unajua alimwambia nini mama Mdogo ili kumshawishi waende wote??
>>>> ‘Mama mdogo twende kuna sehemu Mwanaume amekupenda
anataka kuishi na wewe, alikuona Iringa’ Mama mdogo akakataa na kusema
hajawahi kuishi Iringa, baada ya kuona kagoma akamdanganya kuna watu
wanataka akawafanyie kazi watamlipa vizuri sana ambapo mama mdogo
alishawishika.
5.
Walipofika Lizaboni kwa Mfanyabiashara Sophia alikamatwa sababu taarifa
zilishawafikia Polisi tayari na mpaka sasa anaendelea kuhojiwa,
upelelezi bado unaendelea na ukikamilika atafikishwa Mahakamani kutokana
na biashara hii haramu ya kuuza binadamu.
0 comments:
Post a Comment