Baada ya kuwa na ndoto za kuendesha gari ya kifahari aina ya Lamborghin huku akiwa hana uwezo wa kununua gari hiyo Yu Jietao raia wa Jiangx, China amewashangaza watu wengi baada ya kuja na staili yake ya kutengeneze gari kama hiyo ili atimize ndoto zake.
Jamaa huyo alifikia uamuazi wa kutumia
mbao na kutengeneza gari yenye muundo wa Lamborghin baada ya kuona hana
uwezo wa kumudu gharama za gari hilo zinzofikia Euro 260,000 hivyo
akaamua kufanya hivyo ili kulinganisha na gari hiyo yenye thamani.
Kwa kutumia taaluma yake ya ufundi
seremala Jietao aliamua kutafuta mbao na kutengeneza gari lenye kufanana
kabisa na gari hiyo huku akiweka vifaa vingine vyote vinavyowezesha
gari hiyo kutembea na kufanya kazi kama kawaida.
Muenekano wa gari hiyo umekua kivutio
kikubwa kwa watu wengi huku wakijaribu kutaka kulinunua kwa gharama
kubwa lakini mwenyewe amesema hawezi kuliuza.
0 comments:
Post a Comment