Chid Benzi: kesi yangu fundisho kwangu situmii madawa tenaa

Chid Benz (mwenye shati jeupe) baada ya kuachiwa na mahakama.

MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Rashidi Makwilo maarufu kama ‘Chid Benz’,  aliyekuwa anatuhumiwa kwa kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroin  na bangi, leo ameachiliwa huru kwa kulipa faini ya Sh. 900,000.
Katika maelezo ya awali yaliyosomwa na mwendesha mashtaki wa Jamhuri Diana Lukendo, mbele ya Hakimu Warialwande Lema, msanii huyo  alimwambia hakimu  kuwa mshtakiwa alikamatwa na dawa hizo za kulevya akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl.  Julius  Nyerere,  akitaka kusafiri kuelekea mkoani Mbeya.
Hata hivyo mshtakiwa huyo ambaye alikiri kosa  mnano tarehe 18 Aprili mwaka huu, leo aliiomba mahakama kumpunguzia  adhabu  na kwamba asingetumia tena ulevi huo na atawaelimisha vijana wenzake juu ya madhara yake.
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment