BOSI ALAZIMIKA KUIOMBA MSAMAHA MAITI YA MFANYAKAZI WAKE


Home » General News » Pale ambapo Boss huyu alilazimika kumuomba msamaha marehemu kabla ya mazishi..

January Makamba - Tanzania Mpya

Pale ambapo Boss huyu alilazimika kumuomba msamaha marehemu kabla ya mazishi..

koporsos
Mmiliki mmoja wa bar Kenya alijikuta akilazimika kumuomba radhi marehemu ambaye alikuwa mfanyakazi wake baada ya kutokea tukio ambalo liliwashangaza watu wengi kwenye msiba wa mfanyakazi huyo.
Mashuhuda wanasema mwili wa marehemu huyo ulipakiwa katika gari lakini iligoma kuwaka, waliposhusha jeneza hilo gari liliwaka, watu wakamwambia boss huyo kwamba kama alikuwa na matatizo yoyote na marehemu huyo basi aombe radhi ili waendelee na safari yao salama kwenda kwenye mazishini.
Marehemu huyo ambaye jina lake ni Kamwana alikuwa na ugomvi na mwajiri wake hivyo waombolezaji wakaanza kumsema kwamba bado ana hasira na marehemu huyo.
Boss huyo ambaye ni maarufu kwa jina la Mama Kim alisimama na kumuomba msamaha marehemu; “Kamwana nisamehe kwa yale mabaya niliyokufanyia nami pia nimekusamehea kwa yale uliyonifanyia kwa njia yoyote. Safiri salama.(Kamwana, please forgive me for all the wrongs against you. I also forgive you for offending me in anyway. Have a safe trip),” baada ya maneno hayo walipakia jeneza katika gari hilo likakubali kuwaka.
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment