Hivi ndivyo ilivyotokea kwa mwigizaji, Mercy Johnson baada ya kuwa na marafiki wengi na wengine wanafikia hatua ya kumtembelea nchini Nigeria.
UTAJISIKIAJE pale utakapotambua kwamba umepata marafiki kutoka pande mbalimbali za dunia kutokana na kile unachokifanya?
Hivi ndivyo ilivyotokea kwa mwigizaji, Mercy
Johnson baada ya kuwa na marafiki wengi na wengine wanafikia hatua ya
kumtembelea nchini Nigeria.
Mercy amefanikiwa kuwa na marafiki kutoka Ghana, Liberia, Ufaransa, Uingereza, Marekani, Seychelles na sehemu nyingine nyingi.
“Wengine wakikutana na mimi wanalia, wananipa
maua, zawadi, tunapiga picha, wananiuliza maswali na wengine wanashindwa
kusema chochote na kuishia kutoamini, najua huu ni upendeleo na zawadi
niliyopewa na Mwenyezi Mungu. Miaka michache iliyopita sikuwahi kufikiri
kama nitafikia hatua hii niliyopo leo kwa hili nawashukuru mashabiki,
wadau na tasnia nzima wanaofanikisha haya.”
0 comments:
Post a Comment