Jumapili Dec.14 nchini Nigeria zimetolewa tuzo za Headies Awards 2014
ambazo msanii wa
Tanzania, Diamond Platnumz alikuwa akishindania,
lakini safari hii haikuwa bahati yetu kwasababu hakufanikiwa kushinda.
Sarkodie wa Ghana ndiye aliyeshinda kipengele cha BEST AFRICAN
ARTISTE ambacho Diamond alikuwa akishindania. Wasanii wengine waliokuwa
wakiwania kipengele hicho ni Mafikizolo (South Africa) pamoja na R2Bees
(Ghana).
Hicho ndio kilikuwa kipengele cha kilichoshindaniwa na wasanii wa nje
ya Nigeria kwenye tuzo hizo zilizotolewa Jumapili Dec.14 siku moja
ambayo na Miss World ilifanyika nchini Uingereza.
Katika tuzo hizo Davido alishinda tuzo mbili, ya msanii bora wa mwaka
pamoja na wimbo wake ‘Aye’ ulishinda tuzo ya wimbo bora wa mwaka.
Wizkid alikuwa akishindania kipengele cha msanii bora wa mwaka, tuzo ambayo alishinda Davido.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment