BINTI KUTOKA SOUTH AFRICA ATWAA TAJI LA MISS WORLD 2014






Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amempongeza msichana Rolene Strauss wa A-Kusini alieshinda mashindano ya urembo duniani yaliofanyika jana mjini London huku Chuo kiku anakosemea msichana huyo A-Kusini kikimuandalia hafla kubwa ya kumpongeza atakaporejea nyumbani .
Rolene Strauss aliibuka mrembo wa dunia wa mashindano ya Miss World 2014, akiwashinda zaidi ya warembo 120 kutoka kote duniani.
 
Mshindi huyo wa shindano la Miss World 2014 alivikwa taji la urembo na mshindi wa Miss World 2013, Megan Young kutoka Ufilipino na kushangiliwa na mshindi wa pili na wa tatu, ambao ni Miss Hungary Edina Kulcsár na Miss Marekani Elizabeth Safrit.


Rais Jacob Zuma
Kwa mujibu wa ukurasa rasmi wa mtandao wa Internet, mshindi huyo mwenye umri wa miaka 22 ni mwanafunzi wa mwaka wa nne wa shahada ya udaktari na anafurahia kucheza michezo ya golf, netboli na kuendesha baiskeli na kujisomea vitabu vya burudani na elimu.

Washindi wa tano wa mwanzo katika mashindano ya urembo ya mwaka huu walikuwa kutoka Uingereza, Marekani, Hungary, Australia na Afrika Kusini.
Shindano la Miss World 2014 pia lilikuwa na mshindano tanzu na mataji mengi, ambayo yalifanyika kuelekea siku ya fainali kuu.

Kwa mara ya kwanza, washindani watano walitangazwa kuwa Warembo wa Miss World 2014 wenye Lengo: Washindi hao ni Miss India, Miss Kenya, Miss Brazil, Miss Indonesia and Miss Guyana.
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment