KARRUECHE TRAN HAMTAKII TENA CHRIS BROWN

Karrueche Tran ameapa kutorudiana kamwe na Chris Brown kwakuwa muimbaji huyo wa ‘Loyal’ amekuwa akimuudhi makusudi na kumnyanyasa kiakili.
chris-brown-and-karrueche
Msichana huyo mwenye miaka 26 anasema katika muda wote wa uhusiano wake na Chris amekuwa akinyanyaswa na kwamba hata iweje hawezi kurudiana naye tena. Vyanzo vilivyo karibu na mlimbwende huyo vimesema Chris hajaacha mtindo wake wa kumuumiza makusudi kwa kulike picha za mpenzi wa zamani wa Justin Bieber, Yovanna Ventura kwenye Instagram na kushare picha za Kendall Jenner, 19, akiwa amekaa kwenye mapaja yake.
Anaamini pia Chris alijaribu makusudi kumuumiza kwa kulike picha za Rihanna akiwa na bikini na kuvaa cheni aliyowahi kupewa na muimbaji huyo wa Stay. Karrucehe amedai kuwa hawezi kurudiana na Chris aliyetangaza kwenye show yake huko Los Angeles weekend iliyopita kwa kusema: ”I’m single too! F**k that b***h.”
Wawili hao walianza kuwa wapenzi mwaka 2011 na wamewahi kuachana na kurudiana mara kibao.
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment