Azam iko tayari kuivaa El Merreikh
Klabu
ya Azam ya Tanzania imesema mechi za kirafiki ilizocheza nchini Uganda
hivi karibuni zinatosha kuivaa Klabu ya El- Merreikh ya Sudan katika
michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hapo mwakani.
Azam, wakiwa na
uzoefu wa miaka miwili katika michuano ya kimataifa na kutwaa ubingwa wa
Tanzania Bara kwa mara ya kwanza tangu ianze kucheza ligi kuu Tanzania
bara mwaka 2008, wamepangwa kuwavaa vigogo hao mabingwa mara 19 wa Sudan
na wazoefu wa michuano ya kimataifa katika mechi za awali za mtoano
zitakazochezwa nyumbani na ugenini.Msemaji wa Azam, Jafar Idd amesema hawaoni sababu ya kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kujiandaa na mechi hiyo.
“Safari yetu ya Uganda ilikuwa ni sehemu ya maandalizi ya ligi ya mabingwa pia”, alisema Idd.
Iddi alisema badala ya kusafiri nje ya nje, wataangalia uwezekano wa kualika timu kutoka nje na kucheza Tanzania na si kutoka nje ya nchi.
“Mechi za ligi kuu pia zitakuwa sehemu ya mazoezi ila kifupi tumejiandaa na vitaa hii”, alisema.Iddi alinukuliwa hivi karibuni akisema kocha wao, Joseph Omog kutoka Cameroon amefurahia kupangwa na El Merreikh katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kocha huyo ambaye awali alishawahi kukutana na timu hiyo kipindi cha nyuma akiwa amedai anaifahamu timu hiyo hivyo hana hofu.
Azam ambayo inashiriki kwa mara ya kwanza michuano hiyo imejipanga kuhakikisha inafanya vyema baada ya kusajili wachezaji imara na inatarajiwa kuanza karata yake dhidi ya Wasudan hao kati ya Februari 13-15 mwakani, ikiwa kwenye ardhi ya nyumbani.
“Kocha amefurahia sana ratiba hii na kudai ni nzuri kwetu kwani anaifahamu vyema Al Merreikh na aliwahi kukutana nayo kwenye michuano ya Kagame mwaka jana ingawa walitutoa kwa njia ya mikwaju (penati)”, alisema Idd.
Azam iliweka kambi jijini Kampala, Uganda kwa siku kumi kwa ajili ya mazoezi ya kujiandaa na ligi ya Tanzania itakayoendelea Jumamosi katika raundi ya pili. Ikiwa Uganda, ilicheza na timu vigogo kama vile SC Club Villa na wakusanya ushuru (URA), ambapo mabingwa hao wa Tanzania walifungwa 1-0.
Mechi ya Azam ya marudiano itachezwa baada ya wiki mbili huko Sudan (Kati ya February 27 na Machi 1).
0 comments:
Post a Comment