ALIYEKUA RAISI WA MAREKANI ALAZWA

Aliyekuwa rais wa Marekani alazwa

George H.W Bush
Aliyekuwa rais wa Marekani George H.W Bush amekimbizwa katika hospitali moja ya Houston nchini Marekani baada ya kupatikana na tatizo la kupumua.
Kulingana na madaktari,Bush mwenye umri wa miaka 90 anachunguzwa katika hospitali ya Methodist.
Alipelekwa katika hospitali hiyo na ambalensi jumanne usiku.
Wawakilishi wa Bush wanasema kuwa hatua hiyo ya kupelekwa hospitali ni kama tahadhari.
Rais huyo wa 41 ndio mzee kuwahi kuiongoza Marekani akimshinda Jimmy Carter kwa miezi michache.
Alihudumu kwa muhula mmoja baada ya kushindwa na Rais Bill Clinton.
Bush ambaye hawezi kutumia miguu yake,hivi majuzi alionekana amekaa katika kiti cha magurudumo katika hafla iliofanyika mwezi November katika chuo kikuu cha Texas na mwanawe aliyekuwa rais George W Bush.
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment