COUTINHO ALIA, AOMBA... ULINZI

Mshambuliaji wa Yanga, Mbrazili, Andrey Coutinho.

BAO la mita 20 alilolifunga kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mbrazili, Andrey Coutinho, limempa jeuri na ujasiri wa kuahidi kufunga kila mechi atakayocheza kwenye Ligi Kuu Bara.
Mbrazili huyo aliyetua kuichezea Yanga msimu huu wa ligi kuu kwa mkataba wa miaka miwili, alifunga bao lake a kwanza wakati timu yake ilipocheza na Prisons Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kiungo huyo alifunga bao hilo akitokea kwenye majeraha ya enka baada ya kukosa mechi ya kwanza ya ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar na Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC.
Akizungumza na Championi Jumatano, Coutinho alisema kuwa hayo ndiyo malengo aliyojiwekea msimu huu, anaamini atafanikiwa kutokana na ubora wa kikosi chao. Coutinho alisema, kikubwa anachoomba ni kutopata majeraha makubwa yatakayomsababishia akae nje ya uwanja kama ilivyotokea hivi karibuni.
Aliongeza kuwa, amewaomba waamuzi watakaochezesha mechi zao kumlinda kutokana na mabeki wa timu pinzani kumchezea rafu za makusudi ambazo anaamini zitamsababishia majeraha makali.
“Malengo yangu ni kufunga kila mechi nitakayocheza ndani ya uwanja msimu, malengo yangu ni kutimiza ahadi yangu niliyowapa mashabiki wa Yanga ya kuchukua ubingwa msimu huu wa ligi baada ya kuifungia timu yangu bao la kwanza dhidi ya Mtibwa.
“Ninaamini kama waamuzi wakinilinda dhidi ya mabeki wa timu pinzani wanaocheza kwa kunipania kwa lengo la kuniumiza kwa makusudi, basi malengo yangu hayo ya kufunga katika kila mechi yatafanikiwa.
“Ukiangalia kwenye kila mechi nitakayocheza, hakuna nitakayomaliza salama, lazima nitatoka na majeraha mwilini mwangu, mechi dhidi ya Prisons imemalizika nikiwa nimepata majeraha kwenye misuli yangu ya paja,” alisema Coutinho.
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment