KISUKARI ni moja ya magonjwa yanayoathiri watu wengi siku hizi nchini
mwetu na hata nje. Kati ya hao, wengi huishi na ugonjwa huo kwa muda
mrefu na kuja kugundua kwamba wana kisukari baada ya muda wa kama miaka
mitano hivi, baada ya mwili kuanza kuonesha dalili kuu za kisukari.
Ndani ya kipindi hicho cha miaka mitano, tayari mwili unakuwa umepoteza
baadhi ya uwezo wake katika macho, figo, fizi na neva za fahamu.
Kisukari hakina dawa ya kutibu kabisa, bali vipo vichocheo (hormone) na
dawa zinazosaidia kurekebisha kiwango cha sukari mwilini.
DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI
Baadhi Ya Hizo Ni ;
Kiu Ya Maji Isiyoisha
Njaa Kali,
Kwenda Haja Ndogo Mara Kwa Mara
Vidonda Au Michubuko Kuchukua Muda Mrefu Kupona. Nyingine Ni Ngozi Kuwa Kavu Na Kuwasha,
Mgonjwa Kupoteza Uzito Bila Sababu,
Kuwa Na Ukungu Machoni,
Kuchoka Kusiko Kwa Kawaida,
Hisia Kupungua Katika Vidole Na Viganja Mikononi Na Miguuni Na Kuwa Na
Ukungu Katika Fizi, Ngozi Na Kibofu Cha Mkojo.
Kukosa Hamu Ya Tendo La Ndoa Na Uume Kutoku Simama.
Mwanamke Kujifungua Mtoto Mwenye Uzito Wa Zaidi Ya Kilo Nne Na
Aliyekuwa Na Kisukari Cha Ujauzito Anaangukia Pia Kwenye Kundi Hilo,
Sawa Na Wale Wanaokuwa Wamepata Ajali Na Kuumia Sehemu Za Tumboni Au
Kula Chakula Chenye Sumu Ambacho Kinaweza Kuumiza Kongosho.
MADHARA YA KISUKARI
Watu Wenye Kisukari Wapo Katika Hatari Zaidi Ya Kupatwa Na :
Magonjwa Ya Moyo,
Kiharusi,
Matatizo Na Kuharibika Kwa Kibofu Cha Mkojo,
Shinikizo La Juu La Damu
Upofu
Kufa Neva Za Fahamu,
Uharibifu Katika Fizi Na Ugonjwa Wa Fangasi.
Mtu Anapokuwa Na Kisukari, Mzunguko Wa Damu Miguuni Hupungua Na Hii
Ndiyo Sababu Kubwa Ya Kufa Kwa Neva Za Fahamu Na Hivyo Mtu Kukosa Hisia
Katika Eneo Hilo La Mwili.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment