Baada ya kuingia studio kubwa za Universal kurekodi wimbo huo jana, Donald amesema wimbo huo utatoka wiki Ijayo.
Wakihojiwa kupitia kituo cha radio cha Kaya Fm 95.9 cha Afrika Kusini, Donald akiwa na Diamond kwenye studio za radio hiyo amesema kuwa video ya wimbo huo inatarajiwa kuanza kushutiwa Jumamosi hii.

Donald ameongeza kuwa sababu za kuamua kufanya kazi na Diamond ni kutokana na ukubwa alionao, na baada ya kufanya utafiti wa msanii anayeweza kumtambulisha vizuri Tanzania kwa kufanya naye kazi, bahati hiyo ikamdondokea Diamond. Ameongeza kuwa amewahi kuombwa collabo na wasanii wengi lakini hakuona kama wanaendana kama ilivyokuja kutokea kwa Diamond.
“Hii ni biashara ni muhimu kujua impact ya msanii unayetaka kufanya naye kazi kabla hamjafanya, nilifanya utafiti wangu baada ya kusikia ukubwa wa Diamond Platnumz, nikagundua huyu ndiye msanii nayeweza kuanza naye safari yangu ya kujitangaza Afrika.”
Radio nyingine ya S.A waliyofanyiwa mahojiano juu ya collabo yao ni Metro Fm.
Donald na Diamond pia jana walifanya mkutano na waandishi wa habari kwenye studio za Universal kuhusu ujio wa collabo hiyo.
Sikiliza mahojiano ya Doamond na Donald-Kaya Fm
0 comments:
Post a Comment