Linex amlaumu Adam Juma baada ya video ya ‘Salima’ kutoswa na runinga za nje, AJ ajibu na kueleza sababu

Linex Sunday Mjeda amesema kuwa video yake ya ‘Salima’ aliyomshirikisha Diamond Platnumz imekataliwa kuoneshwa na vituo vikubwa vya runinga vya kimataifa kutokana na kukosa ubora wanaouhitaji.
linex n diamond
Linex amesema kuwa kinachomsikitisha zaidi ni jinsi alivyowekeza pesa nyingi katika utengenezaji wa video hiyo na bado haijafikia kiwango cha kuchezwa na vituo vya nje.
“Unajua sometimes tunakuwa tunalalamika na nini, inafikia point msanii unaamua kuinvest chapaa yako yaani unainvest hela yako kwaajili ya kufanya kazi na director wa ndani na kizalendo unajua. Sasa inapofikia point unapata connection kabisa ya kuweza kutuma labda video yako kwenye vituo vikubwa vya TV halafu vituo vikubwa vya TV vinatoa kasoro ina disappoint sana.” Amesema Linex ambaye hakuwa tayari kutaja gharama iliyotumika kutengeneza video hiyo.
“Kwa mfano video yangu ilipata nafasi ya kuangaliwa na watu ambao wako kwenye music department ya MTV Base, lakini jibu la e-mail iliyorudi ni kwamba wamependa story ya video na wanawish wangeweza kuicheza lakini hawataicheza kwasababu haina ubora ule wanaoutaka.”
Ameongeza kuwa licha ya video ya ‘Salima’ kukataliwa na vituo vikubwa imepata support na kuchezwa na vituo mbalimbali vya ndani kwenye baadhi ya nchi za Afrika.
“Japo saizi nimekuwa napata airtime kwenye local TV za kawaida kama Tv labda za nchi nyingine kama Burundi, Rwanda, Botswana, Zambia, Malawi, Kenya.
Ina disappoint kuona kwamba una invest chapaa halafu unakuja kupeleka video kwenye vituo vikubwa kwa lengo la kupata nafasi halafu labda ile video inakuja inakataliwa so nimekuwa disappointed kwenye hilo. “


“Lakini bado niko na imani na ma-director wa ndani bado nina imani nao kwasababu mi nafikiria video ni investment, kwahiyo labda sikupata ile quality ambayo ilikuwa inatakiwa kutokana na investment yangu labda, japo mimi nimeona nime-invest pesa nyingi nimemlipa Adam hela nyingi kama alivyotaka, lakini labda investment yangu haikustahili Adam ku-hustle kupata ile quality ambayo ilikuwa inaweza kupata airtime kwenye hivyo vituo kwahiyo siwezi kumlaumu na bado nina imani nae.”
Linex amesema kuwa video yake ijayo ana mpango wa kuifanya na director wa nje ya Tanzania.
“Lakini my next video tayari niko na mazungumzo na director mmoja hivi mkubwa sitaki kumtaja sazi ni nani kwaajili ya my next video kwasababu tayari nina wimbo mwingine umeshaisha na mwisho wa mwezi huu nitaanza kushoot kwasababu sitaiacha Salima iende kwa muda mrefu bila kutoa wimbo mwingine juu kwasababu ni wimbo ambao najua utaishi tu hata nikiweka wimbo mwingine Salima haiwezi kuathirika kwasababu ni wimbo ambao uko kwenye maisha ya kila siku ambayo tunaishi.”
“Sija giveup na ma-director wa ndani lakini my next video ntafanya na director wa nje, lakini sio kwamba nikishafanya na director wa nje ndo ntakuwa siwezi kufanya na Adam tena au na Hans au director mwingine anafanya kwa sasa, No naweza kufanya.”

Bongo5 ilimtafuta director Adam “AJ” Juma wa Visual Lab: Next Level aliyefanya video ya ‘Salima’ ya Linex ili kupata maelezo yake, na ametoa sababu za kwanini video ya Linex imekosa ubora uliohitajika na vituo vingi vya nje.
“Najua watu wengi sana wanataka kujua majibu ya video ya Linex. Mimi fee yangu ku-direct video, ku-edit na color correction ni milioni 3, hiyo ni basic package.
Kwa sababu ya mazingira yetu ya kazi kuna wengi ambao hawawezi ku-afford hizo gharama, huwa tuna-include camera (5d mark ii) na basic light package LED 2000 watts, monitor, drives, slider, tripod, transport na crew ya watatu. Ukitaka ubora zaidi msanii anatakiwa ajipange tukodi red ambayo ni kama pesa ya Kenya ksh 80000 au dola 1000 au rand 12000 tsh 1.5- 2Mil , lens nzuri almost $200.” alisema AJ.
“Fee ya director na production haihusiki kwenye kukodi camera au vitu extra ni msanii au mteja mwenyewe. Mtu anayetaka ubora ambao unaendana na viwango vya kimataifa ni bora uwekeze kazi inakuwa rahisi kwa director.”
“Inawezekana mimi nina mapungufu hilo silikatai ila kwa hili la Linex mtakua mnanionea, nayatua maji leo yamwagike tu. Linex alilipa milioni 2 laki 8 na hamsini tu kwa gharama ya kila kitu, ambayo ni chini ya kiwango cha fee yangu, kitu ambacho sio sawa. Anavyosema katumia pesa nyingi sio kweli, labda mambo mengine lakini sio kwa upande wangu, ukipiga hesabu kwenye hiyo pesa utakuta haitoshi ku-cover vitu vingi vilivyohitajika.”
Aliendelea, “Watu mkiwa kwenye Youtube ni rahisi sana kuongea na kushusha maneno bila ya kujua ukweli, kila siku mimi nanyamaza it doesn’t mean it’s right. Nimeshoot video ya Linex na camera hiyo hiyo ambayo ime-shot video ya Christian Bella, Bella aliongeza pesa tukakodi Master prime lens za $750 na tofauti inaonekana bila ubishi.
“Kweli kazi ina mapungufu, nawaomba watanzania mnisamehe, Linex unisamehe kwa hilo nimejitahidi nilipoweza kiukweli imetokea bahati mbaya. Dhumani kubwa mimi kufanya hizi kazi nikufanya msanii aweze kupata maaendeleo sio arudi nyuma kimaendeleo, kwa hayo machache natoa ushauri tu kwa wasanii, ukitaka ubora wa juu usichungulie pesa mzee jipange vizuri hata ukienda kwa GODMAMA huna budget utachekesha tu” Alimaliza AJ.
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment