Hizi ndizo sababu zinazo pelekea kuvunjika kwa mahusiano

Talaka kutokana na utafiti zimeongeza kuanzia miaka ya 1980, na watafiti wa mambo wanasema asilimia 70 ya talaka zote, wapenzi au wanandoa huachana kwasababu ya mambo yaliyokuwepo hata kabla hawajaoana.


Swali ni kwamba kwanini uliamua kuwa na mtu huyo? Kwanini hamkusubiri mpaka kila mmoja wenu awe tayari? Watafiti hao wanasema majibu ni rahisi sana, watu wengi huamua kwa matarajio badala ya kuangalia kile kilichopo kwa muda huo wakiamini mtu huyo atabadilika na mambo yatakwenda vizuri, inawezekana au isiwezekane!

Hakuna dalili ya uchumba yoyote ambayo imekusudiwa kusababisha ndoa isiyo na furaha ila wanandoa wenyewe wana jukumu la kufanya hivyo. Kabla ya kuvunja uchumba huo, lazima muongelee vitu vya msingi vinavyosababisha uchumba huo kuvunjika au kuongea na washauri wenu kama mnao kama hamna washauri mnaenda kichwa kichwa. Lengo la makala hii ni kutusaidia kuwa na uelewa wa mambo fulani ya msingi ambayo tunaendelea kufanya makosa kila siku;

Kunyanyaswa na kufanyiwa ukatili

Kama mwenzi wako aliwahi kukunyanyasa au kukufanyia ukatili, uwe wa matendo, maneno au kihisia inawezekana ikawa moja ya sababu ya kuachana naye. Hata kama hajawahi kukusababishia majeraha, lakini anaonekana kukutawala au kuna matendo ya kutumia nguvu hiyo inaweza kukupelekea kuwa na ugomvi ndani ya nyumba hivyo lazima uchukue tahadhari mapema. Namna ya kushughulikia madhara ya ugomvi wa ndani ni magumu kuliko kuepukana nayo kabla ya kuingia huko, kama amewasha taa nyekundu sasa kwanini ung’ang’anie kuingia?

Kutofanana kimalengo na aina ya tabia

Ingawa inasemekana kuwa hasi na chana mara zote hukutana na kwenda pamoja bali kuna vitu vya msingi huwa vinarudisha nyuma wapenzi wengi, kutokana na utafiti. Vitu hivyo ni kama hawana imani moja lazima wapate shida kwenye ndoa yao kwa kuwa wanaamini vitu tofauti ambavyo vitaathiri maisha yao ya kila siku na hata watoto watashindwa kujua waelekee wapi, hivyo familia inakuwa haijatengamaa. Kuna vitu vidogo vidogo kama kutofautiana mambo ya siasa, hivyo vinaweza kuyafanya mahusiano yetu kuwa yenye mvuto zaidi. Kuna tabia ambazo kama unazichukia sasa na hujaweza kuziweka wazi usitegemee zitaondoka ukifika ndani.

Kuwa na malengo tofauti

Kama mna malengo tofauti vile vile yataathiri maisha ya ndoa. Kama kuna vitu ambavyo havina afya katika mahusiano kama uzembe na uvivu hiyo ni dalili umechagua vibaya. Unatakiwa kuwa na mtu sahihi anayeendana na malengo yako ya maisha , mkitofautiana tu ndani ya nyumba kutakuwa na tofauti nyingi na za kutosha na mwisho wake talaka haitaepukika.

Kukosekana upendo

Ingawa inawezekana unafurahia muda unaotumia na mwenzi wako mtarajiwa na kuonekana kumjali sana haimaanishi unampenda kama mwenzi wa kuishi naye. Kama unaona wewe au mwenzi wako kuna udanganyifu, au kukosa uaminifu kwa wazi kabisa inawezekana ni ishara ya kuvunja mahusiano hayo.

Kutokuwa tayari kwa ajiri ya ndoa

Ndoa ni tendo la makubaliano kati ya wawili na kuwa tayari kuwa na mtu kwa ajili hiyo. Kutokuwa na uhakika kwa kile unachohitaji kwenye maisha yako kama fedha, hisia au kuridhika vitu ambavyo vinakuondolea ujasiri wa kuendelea kwa ajili ya ndoa inakubidi tu muachanane ingawa itakuumiza bali itawasaidia wote wawili baadaye.
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment